Katibu Mkuu
Kilimo Bwana Gerald Kusaya leo tarehe 10 Agosti, 2020 ametoa pikipiki tatu,
trekta moja dogo aina ya ‘Power Tiller’ kwa ajili ya Wanachuo na Wakufunzi wa
Chuo cha Kilimo Maruku (MATI Maruku) cha mkoani Kagera na kuahidi kuwanunulia
basi (Coaster) ili kujibu changamoto ya Wanachuo ya usafiri, pamoja na mafunzo
kwa vitendo (Field Practicum).
Katibu Mkuu
Kusaya amesema, pikipiki hizo tatu zitakabidhiwa muda mfupi kuanzia wiki ijayo
ili ziwasaidie Wakufunzi kutimiza majukumu yao kwa ufanisi.
Wakati huo
huo Katibu Mkuu amesema Wizara ya Kilimo itatoa computer za mezani (Desktop
Computers) pamoja na kufunga mfumo wa maktaba kwa njia ya mtandao (E – Library)
pamoja na kufunga viyoyozi viwili (Sprit Units) kwa ajili ya chumba maalum cha
‘computer’ ya Wanachuo kujisomea.
“Napenda
kuwafamamisha Uongozi wa Chuo cha MATI Maruku pamoja na Wanachuo; mahitaji yenu
yote, Wizara imeyachukua na inafafanyia na itayatolea majibu haraka
iwezekanavyo”.
“Mkuu wa
Chuo andika mahitaji yote na yaje kwa maandishi, mahitaji ya kuboreshewa
miundombinu ya maji pamoja na mfumo vya maji taka kwa vyoo vya mabweni ya
Wanachuo wa Kiume, wiki ijayo nataka kuona Mkuu wa Chuo umewasilisha maombi
haya ya miundombinu ya vyoo vya Wanaume ili ukarabai ukamilike kwa wakati,
ndani ya mwezi huu wa Agosti”. Amekaririwa Katibu Mkuu.
Katibu Mkuu
Kusaya pia ametoa kiasi cha shilingi milioni 10 kwa ajili ya kuanzisha mradi wa
kisasa wa ufugaji wa kuku ambapo kiasi hicho cha fedha kitatumika kwa ujenzi wa
banda la kisasa kufuga kuku kwa ajili.
Mradi huo
utakisaidia Chuo cha MATI Maruku kama chanzo cha mapato kwa ajili ya kusaidia
mahitaji mbambali ya Chuo pamoja na kutumika kama chanzo cha mapato pamoja na
kujifunza dhana ya ujasiliamali.
Aidha
Katibu Mkuu Kusaya ameahidi kutoa fedha kwa ajili ya kugharamia mafunzo ya
nadharia na vitendo kwa Mkufunzi wa MATI Maruku (Bi. Esperance Anatory) ambaye
ataenda kujifunza kuhusu ufugaji wa kuku walioboreshwa katika Kituo cha Mafunzo
cha Silver land eneo la Ihemi, mkoani Iringa, muda mfupi ijao.
0 comments:
Post a Comment