METDO Tanzania

METDO Tanzania

Monday, August 3, 2020

Bilionea Laizer aibua jiwe jingine la Tanzanite





Na Agness Nyamaru
.

Waziri wa madini Dotto Biteko amewataka  wachimbaji wa madini kujiunga katika kuuza  madini kwa uwazi kwani serikali haipo tayari kuona Mtanzania akipunjwa haki yake

Akizungumza wakati wa hafla ya ununuzi wa madini ya Tanzanite kutoka kwa mchimbaji mdogo ,bilionea Saniniu Laizer ,lililopatikana mnamo julai 17 Mwaka huu,Biteko amesema serikali haipo tayari kumpunja Mtanzania haki yake kwani mchimbaji akienda kinyume na sheria hawezi kufanikiwa,kwani mwenye dhana ya kutorosha MADINI hayo hata fanikiwa .

 Aidha Waziri Biteko amesema yeyote atakayechimba madini kwa uhalali hawezi kusumbuliwa na hatua nyingine itakayofuata ni uongezaji wa thamani madini hayo nchini katika maeneo mbalimbali ili biashara ya madini imalizikie masokoni.

 Waziri Biteko amesema eneo la kitalu C liliko mgodi wa mererani lisiguswe kwa sasa na wachimbaji kwani serikali bado inaendelea kufanyia kazi ili waruhusu kuendelea na shughuli ya uchimbaji hivyo eneo hilo bado linalindwa na jeshi la wananchi.

Kwa upande wake waziri wa fedha Philip mpango amesema kuwa katika kuhakikisha huduma za fedha zinapatikana katika eneo husika taasisi zote za fedha zitapatikana katika eneo hilo la machimbo ya Mererani.

Naye billioner Saniniu Laizer amewataka wachimbaji wenzake  kuwa wazalendo kwa kuacha kutorosha madini kwani utaratibu wa serikali ni mzuri na unalenga kumfaidisha kila mchimbaji mdogo.

Hata hivyo  jiwe hilo lenye uzito wa kilo 6.3317 limenunuliwa na serikali kwa  Sh.bilioni 4.846 ambapo katika machimbo ya mererani  kuna zaidi ya migodi 170 kwani mnamo 2017 walifanikiwa kukusanya Million 238, huku baada ya ukuta huo walifanikiwa kukusanya Sh Billioni 1.4 ikiwa mwaka 2019 walifanikiwa kukusanya Sh billioni 1.998 ikiwa Ni sawa na billioni 2.

 

Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com