Afisa uvuvi wilaya Josephine Mazula
akimuonyesha mkuu wa wilaya ya Ikungi Miraji Mtaturu vifaranga vya samaki
vipataavyo 3,500 vyenye thamani ya shilingi laki 9 vilivyopatikana
Kingorowira Morogoro.
Mkuu wa wilaya ya Ikungi Miraji
Mtaturu akisalimiana na afisa uvuvi wilaya Josephine Mazula wakati akionyeshwa
vifaranga vya samaki vilivyotoka Kingorowira Morogoro.
MKUU wa wilaya ya Ikungi mkoani
Singida mhe. Miraji Mtaturu amewataka wananchi kufuata kanuni za uhifadhi
mabwawa kwa kutofanya shughuli za kilimo na ufugaji mita 60 pembezoni mwa
bwawa.
Mtaturu ametoa agizo hilo wilayani
humo wakati wa zoezi la upandaji miti baada ya agizo lake la kupandikizwa upya
kwa vifaranga vya samaki katika bwawa la Muyanji lililopo katika kijiji cha
Kimbwi kata ya Makiungu kutekelezwa.
Katika agizo lake hilo alilowahi
kulitoa mwishoni mwa mwaka jana alipotembelea bwawa hilo alimuelekeza
mkurugenzi wa halmashauri hiyo kutafuta vifaranga vipya ili kuongeza uchumi kwa
wananchi baada ya kuelezwa kuwa samaki wamepungua na wanaovuliwa ni wadogo
sana.
Akizungumza katika zoezi hilo la
upandaji miti mheshimiwa Mtaturu amewaelekeza wananchi kuwa bwawa hilo
litafungwa kwa miezi 6 hadi mwezi agosti mwaka huu ili samaki wafikie kiwango
kinachotakiwa kuvuliwa.
"Tunajua bwawa hili tukilitumia
vizuri na kufuata kanuni za uhifadhi wake tutaongeza uchumi wetu,na kwa
kutambua umuhimu wa bwawa hili mpango wa halmashauri wa baadae ni kuongeza kina
na kutenga bajeti katika mwaka wa fedha wa 2018/2019,"alisema Mtaturu.
Bwawa hilo linaajiri wavuvi zaidi ya
3,000 ambao wanafanya shughuli mbalimbali za kiuchumi.
0 comments:
Post a Comment