Serikali kupitia Wizara ya Maliasili na Utalii imewasilisha rasimu ya kanuni
ya kusimamia watoa huduma katika sekta ya utalii na ukarimu kwa wadau wa sekta
hiyo ili waweze kutoa maoni yao yatakayosaidia katika kuboresha kanuni hizo
ili ziweze kuwasimamia wafanyakazi kwa
kuhakikisha kuwa huduma zinazotolewa zinazokidhi
viwango vya kimataifa kwa watalii.
Akizungumza jana mjini
Dodoma kwenye mkutano uliowakutanisha
wadau wa sekta hiyo kwa ajili ya kupitia
Rasimu ya kanuni hiyo, Naibu Katibu Mkuu
wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Aloyce Nzuki alisema Wizara imeandaa
rasimu hiyo ili kutoa nafasi kwa wadau kuipitia na kutoa maoni yatakayoisaidia katika
kuiboresha.
Akizungumzia moja ya lengo la
kanuni hizo ni kutaka kuwajengea uwezo wafanyakazi wa tasnia hiyo
ili waweza kushindana katika soko la ajira la kitaifa na kimataifa.
Aliongeza kuwa kanuni hizo pia zitasaidia
kuwawekea ulinzi na usalama katika taaluma hiyo pamoja na kuleta
uwajibikaji na uaminifu katika kutoa huduma kwa vile kutakuwa na mfumo wa kuwatambua.
Alisema hatua hiyo ya ukusanyaji maoni imekuja baada ya sekta hiyo ya kukabiliwa na changamoto ya huduma hafifu
zinazotolewa kwa watalii hususani wale wa kimataifa.
Alisema hali hiyo imechangiwa na ukosefu wa chombo cha kusimamia
viwango vya huduma zinazotolewa katika sekta hiyo.
Alisema kumekuwa na malalamiko ya muda mrefu kutoka watalii kuwa
huduma wanazopata ni hafifu.
Awali, Mkurugenzi wa idara ya Utalii, Deograsias Mdamu, alisema
majadiliano hayo ya kuboresha kanuni hizo yatasaidia kuwa na wafanyakazi mahiri
na wenye weledi katika tasnia hiyo.
Aliongeza kuwa, maoni hayo yatapelekea
kuunda kanuni bora na shirikishi zitakazosaidia
katika kuwasimamia wafanyakazi na waajiri katika kutoa huduma bora kwa watalii kwa kila mmoja kwa nafasi
yake.
Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa Chama cha waongoza watalii
Tanzania, Emannuel Mollell aliipongeza Wizara kwa hatua h iliyofikia ya kuandaa
rasimu hiyo kwa vile rasimu hiyo inatoa
muelekeo mzuri katika sekta ya utalii na
ukarimu nchini.
Akichangia maoni Katibu huyo , Emanuel Molleli alisema ni vyema kanuni igusie maslahi ya wafanyakazi kwani
hicho kimekuwa ni kilio chao cha muda mrefu lakini katika rasimu hiyo hakuna kipengele chochote
kilichozungmzia suala hilo.
Aliongeza kuwa wafanyakazi
wa tasnia hiyo kwa ujumla wake wamekuwa
wakilipwa mshahara midogo sana hali inayoplekea kushusha morali katika
kuwahudumia watalii kwa viwango bora.
Kutokana na uwasilishwaji
wa maoni hayo , hali hiyo ilimfanya Mkurugenzi wa Idara ya hiyo, Mdamu
kumjibu kuwa suala hilo litaangaliwa.
Naye, Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dodoma, Bety Begashe wakati
akichangia maoni aliiomba Wizara iiangalie
namna bora itakayosaidia kutoa mafunzo kwa wafanyakazi hao mbali na mitihani
itakayokuwa inafanywa na wanatasnia hao.
0 comments:
Post a Comment