Mfanyabiashara Azim Dewj akizungumza na
waandishi wa Habari (Hawapo pichani ) wakati wa uzinduzi wa kampeni ya
kuchangia damu na kupata jezi mpya kwa mashabiki wa timu za Simba na Yanga,
uchangiaji damu utafanyika kesho tarehe 11/07/2020 MOI.
Mkurugenzi
wa tiba MOI Dkt Samuel Swai akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni ya
kuchangia dam una kuzawadiwa jezi ya Yanga au Simba.
Kuelekea
mechi ya watani wa jadi kati ya Simba na Yanga siku ya Jumapili, Taasisi ya
tiba ya Mifupa MOI kwa kushirikiana na mfanya biashara Azim Dewj pamoja
wadhamini wa Yanga GSM na wadhamini wa Simba kampuni ya Romario Sports 2010
imezindua kampeni ya kuchangia damu ambapo mchangiaji atapatiwa jezi mpya ya
timu anayoishabikia.
Kampeni
hiyo inayokwenda kwa jina la ‘changia damu okoa maisha upate jezi’
inalenga kukabiliana na changamoto ya upatikanaji wa damu salama kwa majeruhi
wa ajali, Watoto wenye vichwa vikubwa , wagonjwa wasiofahamika na wasio na
ndugu pamoja na wagonjwa wengine wenye uhitaji.
Mfanyabiashara
Azim Dewj amesema hii ni awamu ya pili ya kampeni hii ya uchangiaji damu ambapo
awamu ya kwanza mashabiki wa Yanga na Simba waliochangia damu walipata tiketi
za kuingia kwenye mechi ya watani hao wa jadi.
“Nawahamasisha
mashabiki wa timu za Simba na Yanga kujitokeza kwa wingi MOI kuchangia damu ili
kuokoa maisha ya wahanga wa ajali na wengine wanaohitaji , safari hii
ukichangia damu tunakupa jezi mpya ya timu unayoshabikia” alisema
mfanyabiashara Azim Dewj.
Kwa upande
wake Mkurugenzi wa tiba MOI Dkt Samuel Swai amesema mahitaji ya damu MOI ni
chupa 30 kwa siku ambapo kumekua na changamoto ya upatikanaji wa damu
kutokanana na wachangiaji wa hiari kupungua.
Dkt Swai
amesema zoezi la uchangiaji damu litakua siku ya Jumamosi tarehe 11/07/2020
katika eneo la kuegesha magari la kitengo cha dharura cha zamani ambapo zoezi
litaanza saa tatu asubuhi mpaka saa kumi jioni.
0 comments:
Post a Comment