METDO Tanzania

METDO Tanzania

Monday, August 14, 2017

ANNA ABDALLAH AWAPONGEZA GIRL GUIDES KWA KUIWAKILISHA VIZURI TANZANIA NJE YA NCHI

Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Chama cha  Tanzania Girl Guides (TGGA), Anna Abdallah (katikati) akiwa na Girl Guides waliorejea nchini kutoka kwenye programu ya Yess ya kubadilishana uzoefu katika masuala ya uongozi, utamaduni na maadili  katika nchi za Uganda, Madagascar,  Zimbabwe na Zambia. Hapo ilikuwa wakati wa hafla maalumu iliyoandaliwa na TGGA  Dar es Salaam kwa ajili ya kuwapongeza na kupata mrejesho wa walichojifunza walipokuwa kwenye programu hiyo inayodhaminiwa na Norwey.Anna Abdallah aliwapongeza wasichana hao wanne kwa kuiwakilisha vizuri TGGA  na Tanzania katika programu hiyo nje ya nchi.
Kutoka kulia ni Ummy Mwabondo alikwenda Zambia, Farida Mjoge aliyekuwa Uganda,  Elizabeth Betha (Madagascar) na Edna Chembele (Zimbabwe),
Girl Guides hao wakipata msosi wakati wahafla ya chakula cha usiku iliyoandaliwa kwa ajili yao kwenye Hoteli ya Golden Tulip, Oysterbay, Dar es Salaam.
Anna Abdallah akiotoa nasaha na pongezi kwa Girl Guides kwa kuiwakilisha vizuri TGGA NA Tganzania kwa ujumla, ambapo aliwataka watumie mafunzo waliyoyapata kwa kutoa mafunzo kwa wasichana wenzao nchini.
Wakiwa na furahani Kamishna Mkuu wa TGGA, Symphorosa Hangi (kushoto), Anna Abdallah (katikati) na Mjumbe wa TGGA, Agnes Makenya
Katibu Mkuu wa TGGA Tanzania, Grace Shaba akitoa neno la ukaribisho muda mfupi kabla ya Girl Guides waliorejea nchini kutoka nje ya nchi kwenye programu hiyo kuelezea mambo mbalimbali waliyoyafanya na kujifunza
Grace Shaba akiwatambulisha Girl Guides hao
i Ummy Mwabondo akielezea kwa njia ya picha kazi mbalimbali alizokuwa anazifanya alipokuwa Zambia
Mkuu wa Wilaya ya Ilala, ambaye ni Mjumbe wa  Bodi ya TGGA, Sophia Mjema akitoa ufafanuzi wakati Girl Guides wakielezea mafanikio na changamoto ya mafunzo yao nje ya nchi
Girl Guides Farida akielezea mambo mbalimbali aliyoyafanya akiwa Uganda kwa muda wa miezi sita.
Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com