Wajumbe wa
Kamati ya usimamizi wa Mradi wa uboreshaji wa Taasisi za usimamizi wa
Rasilimali Asilia na Ukusanyaji wa Mapato (PSC)unayofadhiliwa na Benki ya
Maendeleo ya Afrika (AfDB) kwa kushirikiana na Serikali,wakiwa katika picha ya
pamoja walipofanya ziara ya kukagua ujenzi na ufungaji wa Midaki (Scanner)
kubwa na ya kisasa Afrika ya kukagua ya mizigo inayopita katika bandari ya Dar
Es Salaam.Katikati ni Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Kamshina wa Petroli na Gesi wa
Wizara ya Nishati, Adam Zuber, Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Maendeleo ya
Petroli Tanzania (TPDC), Dkt. James Mataragio(pili kulia) na Meneja mradi huo wa Shirika la Maendeleo ya Petroli(
TPDC), Mjiofizikia Asiadi Mrutu(kulia)
Wajumbe wa
Kamati ya usimamizi wa Mradi wa uboreshaji wa Taasisi za usimamizi wa
Rasilimali Asilia na Ukusanyaji wa Mapato (PSC)unayofadhiliwa na Benki ya
Maendeleo ya Afrika (AfDB) kwa kushirikiana na Serikali,wakipata maelezo ya
ufanyaji kazi wa Midaki (Scanner) kubwa na ya kisasa Afrika ya kukagua mizigo
inayopita katika bandari ya Dar Es Salaam, walipofanya ziara ya kukagua ujenzi
na ufungaji wa midaki hiyo Julai 9,2020.Katikati ni Mwenyekiti wa Kamati hiyo,
Kamshina wa Petroli na Gesi Wizara ya Nishati, Adam Zuber.
Wajumbe wa
Kamati ya usimamizi wa Mradi wa uboreshaji wa Taasisi za usimamizi wa
Rasilimali Asilia na Ukusanyaji wa Mapato (PSC)unayofadhiliwa na Benki ya
Maendeleo ya Afrika (AfDB) kwa kushirikiana na Serikali,wakitoka kukagua
maendeleo ujenzi na ufungaji Midaki (Scanner) kubwa na ya kisasa Afrika ya
kukagua mizigo inayopita katika bandari ya Dar Es Salaam, walipofanya ziara
hiyo Julai 9,2020.
Kamati ya
usimamizi wa Mradi wa uboreshaji wa Taasisi za usimamizi wa Rasilimali Asilia
na Ukusanyaji wa Mapato (PSC)unayofadhiliwa na Benki ya Maendeleo ya Afrika
(AfDB) kwa kushirikiana na Serikali imeridhishwa na kasi ya ufungaji wa Midaki
(Scanner) kubwa na ya kisasa Afrika katika bandari ya Dar Es Salaam inayotumia
mionzi kukagua mizigo.
Mradi huo
upo chini ya Wizara ya Nishati ambao unasimamiwa na kutekelezwa na Shirika la
Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) kuanzia ngazi ya manunuzi: Ujenzi wa jengo
la Midaki hiyo umekamilika kwa 99%, kazi ya usimikaji na ufungaji wa vifaa
imekamilika kwa 51%, ambapo inatarajiwa kukamilika mwezi Septemba 2020, kwa
gharama ya zaidi ya Dola za kimarekani milioni 5, zikiwemo na fedha za
kitanzania.
Hayo
yameelezwa na Kaimu Mwenyekiti wa kamati hiyo,Kamishna wa Petroli na Gesi wa
Wizara ya Nishati,Adam Zuber, kwa niaba ya Mwenyekiti wa Kamati hiyo,ambaye ni
Katibu Mkuu Wizara ya Nishati, Mhandisi Zena Said, walipofanya zaira ya kukagua
maendeleo ya ufungaji wa midaki hiyo katika bandari ya Dar es salaam, Julai
7,2020.
Zuber
alisema kuwa midaki hiyo itakapokamilika itakuwa na uwezo wa kukagua magari makubwa
ya mizigo mia mbili kwa saa, hivyo karahisisha utendaji kazi katika bandari
hiyo na kuwatoa huduma kwa haraka kwa wateja.
Midaki hii
itakuwa na uwezo wa kubaini aina mbalimbali za mizigo inayongia na kutoka nje
ya nchi kupitia bandari hiyo, kuondoa udanganyifu uliokuwa unafanya na baadhi
ya wafanyabiashara wasiowaaminifu waliokuwa wakipitisha bidhaa tofauti na zile
zilizoelezwa katika nyaraka husika.
Alisema
kuwa midaki hiyo pia,itaongeza kwa kiasi kikubwa kasi ya ukusanyaji mapato ya
serikali kwa kuwa itakuwa na uwezo mkubwa wa kubaini na kukagua kila kitu
kilichomo katika shehena ya mzigo ili ilipiwe kodi stahiki.
“Hii
Midaki(scanner) ni muhimu sana kwa taifa letu, itarahisisha ukusanyaji wa
mapato, kubaini kilichobebwa ndani ya gari, na kusafirisha mizigo kwa haraka
zaidi, kimsingi kamati imeridhishwa na kasi ya ujenzi wake,na tunaipongeza sana
TPDC kwa kazi nzuri,hii ni midaki(Scanner) kubwa na ya kisasa kwa nchi za
Afrika,”alisema Zuber.
Kwa upande
wake Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC),
Dkt. James Mataragio, aliwahakikishia watanzania kuwa anaimani midaki hiyo
itakamilika kwa wakati kama ilivyopangwa kwa kuwa asilimia kubwa ya utekelezaji
wa mradi huo imekamilika.
Vilevile
alieleza kuwa, midaki hizo mpya zitazotumia teknolojia ya kisasa zitaboresha ukusanyaji wa mapato
serikalini na kurahisisha utendaji kazi katika kukagua mizigo mingi itakayokuwa
ikipita kwa wakati mmoja na kwa haraka zaidi.
“Mionzi
iliyopo katika midaki hii haitakuwa na madhara kwa watumiaji kwa sababu
wakandarasi wanaoijenga wamezingatia na kufuata sharia na taratibu za afya na
usalama sehemu za kazi, hivyo nawatoa hofu watu wote juu ya hili, kuwa
hakutakuwa na hatari zozote za kiafya kwa watumiaji,” alisema Dkt. Mataragio.
Naye Meneja
wa mradi huo, Mjiofizikia Asiadi Mrutu wa TPDC ,alisema kuwa mbali na ujenzi wa
midaki hiyo, pia wataboresha mifumo ya utendaji kazi katika bandari zote
nchini, viwanja vya ndege,pamoja na kuondoa shehena za mizigo zilizopo
mipakani.
Aliweka
wazi kuwa wanufaika wa mradi huo unaofadhiliwa na AfDB ni Wizara ya Nishati, Shirika la
Maendeleo ya Petroli Tanzania ( TPDC), Mamlaka ya Mapato Tanzania ( TRA),
Mamlaka ya Huduma za Nishati na Maji ( EWURA) na Bodi ya Mapato Zanzibar(ZRB).
Wengine ni
Mamlaka ya Udhibiti wa Mkondo wa Juu( PURA),Baraza la Uwezeshaji la Taifa( NEEC
), Mamlaka ya Huduma za Nishati na Mafuta Zanzibar(ZURA), pamoja na Mamlaka ya
Ukusanyaji Mapato Zanzibar( TRA-ZANZIBAR.)
0 comments:
Post a Comment