Jeshi
la Kujenga Taifa (JKT) limetangaza majina ya vijana waliohitimu kidato cha sita
kutoka shule zote za Tanzania Bara
waliochagulwa kujiunga na mafunzo
ya Jeshi hilo kwa mujibu wa sheria ya mwaka 2020 .
Akizungumza
leo Julai 16, 2020 Makao Makuu ya Jeshi
hilo Wilayani Chamwino
Mkoani Dodoma, Mkuu wa Tawi la Utawala, Jeshi la Kujenga
Taifa (JKT) Kanali Julius Kadawi amesema
kuwa Mkuu wa JKT Meja Jenerali Charles
Mbuge anawakaribisha
waliochaguliwa kujiunga na vijana
wenzao katika kujifunza uzalendo, umoja wa kitaifa, stadi za kazi, stadi za
maisha , utayari wa kulijenga na kulitumikia Taifa kupitia mafunzo hayo.
“Orodha
kamili ya majina ya vijana waliochaguliwa, maeneo ya makambi ya JKT
waliyopangiwa na vifaa wanavyotakiwa kwenda navyo inapatikana katika tovuti ya
JKT ambayo ni www.jkt.go.tz”,
Alisisitiza Kanali Kadawi.
Aidha,
Kanali Kadawi amesema kuwa vijana hao wanatakiwa kuripoti makambini kuanzia
tarehe 24 hadi 27 Julai, 2020 ambapo mafunzo yatafunguliwa rasmi Agosti 1,
2020.
Akifafanua,
Kanali Kadawi amesema kuwa kwa upande wa wahitimu wenye ulemavu wa kuonekana
kwa macho (Physical disabilities) wanatakiwa kuripoti
katika kambi ya JKT Ruvu iliyopo Mlandizi mkoani Pwani ambayo ina miundombinu
ya kuhudumia watu wa jamii hiyo.
“Kutokana
na Ugonjwa wa Homa kali ya Mapafu (COVID -19) nchini, Tahadhari za kuzuia
maambukizi ya ugonjwa huo kama ilivyoelekezwa na Serikali kupitia Wizara ya
Afya zitazingatiwa kwa kipindi chote vijana watakapokuwa katika mafunzo”,
Alisisitiza Kanali Kadawi.
Vijana
waliochaguliwa wamepangiwa katika kambi
za JKT Rwamkoma- Mara, JKT Msange- Tabora, JKT Ruvu-Pwani, JKT Mpwapwa
Dodoma, JKT Mafinga- Iringa, JKT Mlale-Ruvuma, JKT Mgambo na JKT Maramba-
Tanga, JKT Makuyuni- Arusha, JKT
Bulombora, JKT Kanembwa, JKT Mtabila- Kigoma, JKT Itaka- Songwe, JKT Luwa na
JKT Milundikwa- Rukwa, JKT Nachingwea- Lindi,JKT Kibiti na Oljoro- Arusha.
0 comments:
Post a Comment