Mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya uchakataji nguzo za umeme ya Qwihaya General Enterprises Company Ltd Leonard Maheda akimueleza jambo waziri Kairuki alipofanya ziara katika kiwanda hicho kilicho mkoani Iringa wilaya ya Mufindi
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri mkuu,Uwekezaji Angellah Kairuki akitete jambo na Mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya uchakataji nguzo za umeme ya Qwihaya General Enterprises Company Ltd Leonard Maheda pamoja na mbunge wa jimbo la Mafinga Mjini Cosato Chumi
NA FREDY MGUNDA,MAFINGA.
Waziri wa Nchi
Ofisi ya Waziri mkuu,Uwekezaji Angellah Kairuki awataka wawekezaji wazawa kuiga mfano
wa kampuni ya uchakataji nguzo za umeme ya Qwihaya General
Enterprises Company Ltd kwa kuwekeza mtaji mkubwa wenye tija kwa
watanzaji na serikali kwa ujumla kutoka na uwekezaji wake kujikita katika miji
ambayo inakuwa kiuchumi.
Waziri
Kairuki alieeleza kufurahishwa na kasi ya uwekezaji inayofanywa na
kampuni hiyo kwa kuwekeza viwanda vya nguzo
katika mikoa mbali mbali ukiwemo mkoa wa Kigoma na
kutaka wadau wengine kuelekeza nguvu zao
katika mkoa wa Kigoma badala ya kuwekeza Dar es Salaam
,Dodoma na mikoa mingine ambayo ni rahisi kufikika .
Kairuki alisema kuwa amefurahishwa na kampuni hiyo kwa kuamua kuwekeza
kiwanda katika mkoa wa Kigoma upo pembezoni mwa
nchini na wawekezaji wengi wamekuwa wakikwepa
kuwekeza viwanda vyao katika mkoa huo
kutokana na umbali ila kampuni hiyo ya Qwihaya imefanikiwa kuwekeza
kiwanda cha kuchakata nguzo za umeme kama ilivyo katika mkoa wa Iringa.
“Nimesikia kwenye risala yenu kuwa hivi
karibuni mtafungua kiwanda katika mkoa wa Kigoma na Njombe jambo ambao zuri kwa
kuwa mnaendeleza kukuza uchumi pamoja na kuongeza ajira kwa wananchi wengi hasa
vijana ambao wamekuwa hawana ajira rasmi” alisema
Alisema kuwa mkoa wa
Kigoma upo pembezoni na serikali imejipanga kuendelea
kuhamasisha wawekezaji kufika kuwekeza katika sekta
mbalimbali katika mkoa
huo kwa kuwa unakuwa kwa kasi kiuchumi na unamazingira mazuri ya uwekezaji
hivyo wadau wanakaribishwa kuwekeza Kigoma.
"Kitendo cha Qwihaya
kufika kuwekeza Kigoma ni uzalendo wa hali ya
juu na mmefungua mlango kwa wawekezaji
wengine kufika kuwekeza katika mkoa wa Kigoma wanahitaji
kunufaika na sekta ya uwekezaji sio kwamba siwapongezi
kwa kuwekeza kiwanda hapa Mafinga mkoani Iringa
nawapongeza pia ila kwenda Kigoma mmefanya jambo
zuri zaidi maana kupitia mkoa wa Kigoma mtakuwa na
uwezo wa kuuza bidhaa zenu katika nchi za jirani na Tanzania
"
Kairuki alisema mpango wa kampuni ya
Qwihaya wa kufungua kiwanda cha kutengeneza dawa
ya kutibu nguzo Kibaha ambacho kitakuwa ni
kiwanda cha kwaza cha aina hiyo kwa Tanzania
kwani alisema kwa sasa hakuna kiwanda cha
dawa ya kutibu nguzo nchini .
Akizungumzia changamoto za
miundo mbinu ya barabara ya Mgololo Mufindi alisema kuwa
tayari TANROADS mkoa wa Iringa wamekwisha fanya
upembuzi yakinifu juu ya barabara hiyo na wakati
wowote itafanyiwa matengenezo ya kiwango cha lami .
Kwa upande wake mkurugenzi
mtendaji wa kampuni ya Qwihaya Leonard Maheda alisema
kuwa kiwanda hicho kimeanzishwa mwaka 2007
kama kiwanda cha uchanaji mbao na mwaka 2015
kilianza kutengeneza nguzo baada ya kauli mbinu ya
Rais Dkt John Magufuli juu ya serikali ya
viwanda na hata kuzuia nguzo kutoka nje ya nchi .
Alisema kuwa kiwanda
hicho kwa mwaka kinauwezo wa kuzalisha nguzo 800,000 na
kuwa nchi nzima wanamiliki viwanda vitatu
vya nguzo na wanakusudia kuanzisha kiwanda
cha dawa za nguzo ambacho kitakuwa kiwanda
pekee cha dawa za nguzo Tanzania .
Awali akisoma taarifa ya
kiwanda hicho kwa waziri Kairuki ,kaimu
mkurugenzi wa kampuni ya Qwihaya General Enterprises
Ltd Benedicto Mahenda alisema kuwa gharama
za uwekezaji wa kiwanda hicho ni takribani kiasi
cha shilingi bilioni 15.
Alisema kuwa kwa kipindi
kirefu kampuni imekuwa ikinunua malighafi za
nguzo kutoka katika shamba la miti la Sao Hill
iliyopo chini ya TFS na wamekuwa wakipata
ushirikiano mkubwa kutoka kwa uongozi wa shamba hilo .
alisema kuwa soko la nguzo
wamekuwa wakitegemea zaidi soko la ndani kupitia mteja
mkubwa shirika la umeme Tanzania (TANESCO) na katika kipindi cha
hiki cha utekelezaji wa mradi wa umeme
vijijii (REA) awamu ya tatu) soko la nguzo limekuwa ni kubwa
sana.
Naye mbunge wa jimbo la Mafinga Mjini Cosato Chumi
alimpongeza muwekezaji wa kiwanda hicho kwa kuwa mzalendo kwa kuchangia
shughuli za kimaendeleo katika sekta mbalimbali katika jimbo la Mafinga Mjini.
“Mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya
Qwihaya Leonard Maheda amekuwa msaada mkubwa kwenye maendeleo ya jimbo langu
kwani ametusaidia kuweka umeme kwenye shule zote za msingi na kusaidia kukuza
sekta ya elimu kuanzia chini hadi ngazi ya sekondari”alisema Chumi
Chumi alisema kuwa kampuni hiyo imekuwa
ikifanya kazi kwa weredi mkubwa kiasi kwamba hakuna malalamiko yoyote yale
kutoka kwa wafanyakazi wa kampuni hiyo tufauti ilivyo kwenye kampuni nyingine
ambazo zimewekaza katika halmashuri ya Mji wa Mafinga.
0 comments:
Post a Comment