Katibu
Mkuu Wizara ya Viwanda na Biashara Prof. Riziki Shemdoe amefungua kikao kazi
cha wataalamu kutoka taasisi mbalimbali za serikali na sekta binafsi ambao
wamekutana kwa ajili ya mapitio ya Sera ya Viwanda Vidogo na Biashara Ndogo
(SME Policy 2003).
Prof.
Shemdoe amesema kwamba Wizara ya Viwanda na Biashara kwa sasa inatekeleza
andiko la kuboresha mazingira ya Biashara nchini “Blue print” ambayo imeondoa
vikwazo vya kibiashara na kuweka mazingira mazuri kwa wajasiliamali, wawekezaji
na wafanyabiashara wote kwa ujumla hivyo kikosi kazi hiki kitasaidia Wizara
kuwa na Sera bora ambayo itazingatia hali ya sasa kwani Sera iliyopo ambayo ni
ya mwaka 2003 mambo mengi yamepitwa na wakati hivyo kushindwa kutatua
changamoto nyingi zinazowakabili wajasiliamali wadogo nchini ambao ndio chachu
ya kuchochea uchumi wa nchi.
"Nafasi
za ajira nyingi zipo kwa wajasiriamali wadogo hivyo Sera hii itasaidia kutatua
changamoto za wafanyabiashara wetu hasa katika suala la upatikanaji wa mikopo
yenye riba na masharti nafuu ili kuwawezesha kufanya biashara katika masoko ya
ndani na nje ya nchi yakiwemo masoko ya COMESA, SADC, EAC n.k ,"
alisisitiza Prof. Shemdoe.
Prof.
Shemdoe amepongeza jitihada zinazofanywa na Mfuko wa Kuendeleza Sekta ya Fedha
Nchini (FSDT) hapa nchini kwani ndio waliofanikisha kikosi kazi hiki kukutana
na kufanya kazi hii ya mapitio ya maandiko mbalimbali ili kurejea Sera ya
Viwanda Vidogo na Biashara ndogo. Pia ameipongeza Sekta binafsi katika
kushirikiana na Wizara ya Viwanda na Biashara katika marejeo ya sera hii kwani
sekta binafsi ndio nguzo ya kusaidia wajasiliamali wadogo nchini kujikwamua.
kwa ushirikiano huu tunatarajia kupata Sera bora na wezeshi kwa wafanyabiashara
wadogo ambao ndio kundi kubwa lililojiali.
Aidha
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Sekta Binafsi
Tanzania (TPSF), Godfrey Simbeye
amesema kuwa yeye na taasisi anayoiongoza ameipongeza Serikali kupitia Wizara
ya Viwanda na Biashara kwa kuja na mapitio ya Sera hii ambayo ni ya mwaka 2003
hivyo Sera mpya itakayopatikana itatoa mwongozo wa Wafanyabiashara wadogo.
Aliongeza
kwa kusema kuwa Sera hii ina umuhimu mkubwa kwa mstakabali wa maendeleo ya nchi
yetu kwani Wafanyabiashara wadogo ndio nguzo ya uchumi ya taifa letu hivyo Sera
mpya inatakiwa kuwa wezeshi kusaidia Wajasiriamali wote nchi nzima.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Mfuko wa Kuendeleza Sekta ya Fedha Nchini (FSDT) Bw. Sostenes Kewe
amesema Wafanyabiashara wadogo ndio injini ya uchumi wan chi hii na mitaji ndio
changamoto kubwa ya kuwafanya kuendelea kibiashara, ujio wa sera mpya itasaidia
kutengeneza mazingira bora kwa wajasiliamali, Napongeza Juhudi zinazofanywa na
Serikali ya Tanzania za kuboresha na kujenga miundombinu hasa ya barabara,
Afya, maji na Umeme zimesaidia sana wajasiriamali kusogea kutoka eneo moja
kwenda eneo jingine kimaendeleo.
Naibu
Katibu Mkuu, Wizara ya Viwanda na Biashara Ludovick Nduhiye akimkaribisha
Katibu Mkuu katika Ufunguzi wa Kikao kazi hiki cha mapitio ya Sera ya Viwanda
Vidogo na Biashara Ndogo (SME Policy) ameishukuru Sekta binafsi (TPSF) pamoja
na Mfuko wa Kuendeleza Sekta ya Fedha Nchini (FSDT) kwa kusema kuwa “hiki
kinachofanyika leo ni matokeo mazuri ya ushirikiano uliopo na unaoendelea kati
ya Serikali na Sekta binafsi katika kutatua changamoto kwa Wajasiriamali
nchini”.
Kikao
kazi hiki kinafanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Nashera Mkoani Morogoro.
0 comments:
Post a Comment