
Mwenyekiti wa umoja wa vijana wa chama Cha mapinduzi (UVCCM)Taifa,amewataka viongozi wa ngazi mbalimbali kutimiza majukumu yao
Na Agnes Geofrey
Mwenyekiti wa umoja wa vijana wa chama Cha mapinduzi (UVCCM)Taifa,Kheri James amewataka viongozi wa ngazi mbalimbali wa chama hicho kutimiza majukumu yao Katika vikao ili watu wapate haki zao kwa kupata mahali pakusemea changamoto zao.
Akizungumza Katika kikao Cha chama hicho wilayani Arumeru,James amesema Ni muhimu viongozi wakatimiza majukumu yao ya kuandaa vikao ili watu wa chini wapate sehemu ya kusemea na kukosoa kwani wasipofanya hivyo watakuwa wanawanyima haki zao za kujadili ajenda.
"Katika kikao hicho msiwanyime wajumbe haki zao za kutoa maoni na Uhuru wa kuongea kwani kiongozi asipofanya hivyo atakuwa anamnyima haki mjumbe wa kikao hicho haki yake kwani hatakiwi kunyanyasika ikiwa hata mawazo yake ni mabaya inabidi asikilizwe kwanza na sio kumnyamazisha".
Pia James amewataka viongozi kuwa na mahusiano mazuri na watu wote ili kujenga umoja na mshikamano ambao utakao waweka pamoja kuleta maendeleo chanya kwa kujadili ajenda moja.
"vitu vinavyaoathiri vikao vya chama hichi ni baadhi ya wajumbe kuwa na vikao baada ya kikao na kikao kabla ya kikao kuja na msimamo baada ya mtazamo, kiongozi kutoheshimu maazimio ya kikao na kukosoa pamoja na kutokuwa na Siri ya kikao."
Aidha James ameongeza kusema kuwa Ni vyema viongozi wafanye ziara ili kuwafikia walenga na kutambua changamoto zao kwani wakifanya hivyo itasaidia kupunguza uongo Katika utekelezaji wa miradi mbalimbali,pia itamsaidia kiongozi kupata uhalisia wa ajenda ya kikao walichojadili.
Naye Mwenyekiti wa UVCCM mkoa wa Arusha Omary Lumato amesema kuwa mwaka huu hawatazembea Katika uchaguzi Mkuu bali watahakikisha Arumeru inarudi CCM, kwani wanasubiri vikao halali vya chama.
Pia Lumato amesema kuwa yeyote atakayeteuliwa Kama kijana ili kufanya kazi ,hawatakuwa na nongwa nae bali watashirikiana kwa pamoja ili kuweza kuleta maendeleo Katika nchi ya Tanzania.
[6/15, 3:51 PM] Agnes: Tittle :Mwenyekiti wa umoja wa vijana wa chama Cha mapinduzi (UVCCM)Taifa,amewataka viongozi wa ngazi mbalimbali kutimiza majukumu yao.
0 comments:
Post a Comment