Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na
Utawala Bora, Jaji Mstaafu Mathew Mwaimu (wa tatu kulia) akizungumza jambo
katika kikao kifupi na Mkurugenzi wa Mashtaka wa Serikali ya Mapinduzi
Zanzibari, Ibrahim Mzee Ibrahim (wa kwanza kushoto), alipomtembelea ofisini
kwake Mjini Unguja Zanzibari Juni 5, 2020, Kulia ni Kamishna Mkazi wa Haki za
binadamu na Utawala bora kwa upande wa
Zanzibari, Khatibu Mwinyichande na Makamu Mwenyekiti wa Tume hiyo, Mohamedi
Khamis Hamadi
Mkurugenzi wa Mashtaka wa Serikali ya
Mapinduzi ya Zanzibari, Ibrahim Mzee Ibrahim(wa kwanza kushoto) akizungumza na ugeni wa Tume ya Haki za
Binadamu na Utawala Bora walipomtembelea
ofisini kwake Mjini Unguja, Zanzibari na kufanya kikao kifupi kuhusu
masuala ya haki za binadamu, kulia ni
Mwenyekiti wa Tume hiyo, Jaji Mstaafu Mathew Mwaimu na Makamu
Mwenyekiti, Mohamedi Khamis Hamadi.
Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu
, Mohamedi Khamis Hamadi akifafanua jambo kwa Mkurugenzi wa Mashtaka wa
Serikali ya Mapinduzi, ya Zanzibari (
hayupo pichani), kuhusu haki za binadamu walipomtembelea ofisini kwake Mjini
Ungua, Zanzibari Juni 5, 2020., kulia ni Kamishna Mkazi wa Haki za binadamu na
Utawala bora kwa upande wa Zanzibari,
Khatibu Mwinyichande na kushoto ni Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na
Utawala Bora, Jaji Mstaafu Mathew Mwaimu
Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na
Utawala Bora, Jaji Mstaafu.Mathew Mwaimu akizungumza na watendaji wa juu wa
tume hiyo na Mkurugenzi wa Mashtaka wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibari,
Ibrahim Mzee Ibrahim, wakati wa kikao kifupi kuhusu haki za binadamu
kilichofanyika ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka Mjini Unguja Zanzibari Juni 5,
2020.
Mwenyekiti
wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Jaji Mstaafu Mathew Mwaimu amesema
kuwa ushirikiano baina ya Tume hiyo na Serikali ni Muhimu ili kutekeleza majukumu
ya kuwapatia wananchi haki inayohitajika katika masuala mbalimbali ya jamii.
Akizungumza
katika Ziara aliyoifanya Ofisi ya Mkurugenzi wa
Mashtaka iliyopo Mjini Unguja, Zanzibari Jaji Mwaimu alisema kuwa tume
ya haki za binadamu ni chombo cha serikali ambacho kipo kisheri kwa ajili ya
wananchi kikilenga ukuzaji na ulindaji wa haki
kwa pande zote mbili.
“Tume ni
chombo cha Serikali ambacho kipo kisheria na majukumu yake ni kukuza na kulinda
haki za binadamu na misingi ya utawala bora kwa Serikali na wananchi, tunafanya
kazi ya kuisaidia Serikali maana yake pande zote mbili viongozi na wananchi kwa
kushughulikia malalamiko mbalimbali ya
pande hizo”, Alisema Jaji Mwaimu.
Alisema
kuwa lengo kuu la ziara ya kupita kila ofisi inayohusiana na masuala ya utekelezaji
wa haki za binadamu ni kujenga mahusiano bora katika kitumiza azma ya
kuiwezesha Serikali kujua mahali ambapo kuna ukiukwaji wa haki za binadamu ili
iweze kutatua jambo hilo kwa haraka zaidi.
Naye,
Mkurugenzi wa Mashtaka wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibari, Ibrahim Mzee
Ibrahim alisema kuwa ataendelea kutoa ushirikiano kwa ofisi ya Tume hiyo kwa
kuwa utekelezaji wa majuku yake unaendana na uwepo wa haki za binadamu.
“Majukumu
ya ofisi yetu tunayoyafanya kila siku, mara nyingi yanahusiana sana na haki za
binadamu kwa sababu mtu akikutwa na jinai yeyote moja kwa moja lazima haki yake
iangaliwe na hukumu itolewa kwa kuzingatia sheria na haki za binadamu, kwa hiyo
ushirikiano wetu na ofisi ya tume unahitajika sana na mimi nasema tutaendelea
kutoa ushirikiano kwa ofisi yako”,
alisema Ibrahim Mzee.
Aliongeza
kuwa tume hiyo imepewa jukumu kubwa la kutekeleza na kuleta haki za binadamu,
kwani imekuwa msaada mkubwa kwa Serikali na wananchi katika kulinda na kuweka
hali sawa kwa malalamiko mbalimbali.
“Tume
mumepewa jukumu zito, lakini naamini jukumu limefika kwenye mikono salama kwani
mnakwenda vizuri na kasi ya Serikali ya Awamu ya Tano, na mumeleta heshima kwa
tume hii na sasa inafanya kazi kwa manufaa makubwa ya wananchi na Serikali
yao”, Alifafanua Ibrahim Mzee.
Kwa Upande
wake Makamu Mwenyekiti wa Tume hiyo, Mohamedi Khamis Hamadi alisema kuwa tume
imeendelea kushirikiana vizuri na ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka Zanzibari
katika kuleta haki kwa wananchi na aliomba kuwepo na mashirikiano mbalimbali yakiwemo
ya mafunzo kwa watumishi wa ofisi hizo mbili.
0 comments:
Post a Comment