METDO Tanzania

METDO Tanzania

Saturday, June 6, 2020

WADAU WA MICHEZO ILEMELA WAJADILI UENDESHAJI WA MASHINDANO KIPINDI CHA UGONJWA WA CORONA.

Wadau wa michezo katika manispaa ya Ilemela wamekutana kujadili juu ya namna bora ya kuendesha mashindano mbalimbali ya kimichezo wakati wa maambukizi ya ugonjwa wa Covid-19 unaoenezwa na kirusi cha Corona.

Akizungumza katika ukumbi wa uwanja wa CCM Kirumba kwenye kikao cha kujadili utekelezaji wa shughuli za kimichezo wakati wa janga la ugonjwa wa Covid-19,  Afisa Michezo wa manispaa Ilemela Ndugu Bahati Kizito Sosho amesema kuwa maambukizi ya ugonjwa wa Covid-19 kwa kiasi kikubwa yamepungua  tofauti na hali ilivyokuwa hapo awali kwa mujibu wa maelekezo ya  wataalamu wa afya huku akisisitiza kuwa ugonjwa huu umekuwa ukiathiri zaidi watu wasiopenda kufanya mazoezi ya kimichezo

'.. Tuna Rais mchapa kazi anapenda michezo, Na hivi punde ameruhusu mashindano ya michezo yaweze kuendelea, Sasa sisi wasaidizi wake tuna wajibu wa kuwaanda watu wetu kuchukua tahadhari wakati mashindano yakiendelea .. ' Alisema

Aidha Ndugu Kizito akawataka wadau  wa michezo kuhakikisha wanajisajili katika Virabu vya michezo wanayoishiriki ili kuzitambua na kuleta urahisi wa kusaidia timu inayofuzu mashindano rasmi ya kitaifa na kimataifa 

Kwa upande wake mratibu wa elimu juu ya magonjwa kwa wananchi Bi Rose Nyemela amesisitiza kuwa ugonjwa bado upo hivyo wananchi waendelee kuchukua tahadhari ya kujikinga na ugonjwa huo ikiwemo kunawa mikono mara kwa mara, kutumia vitakasa mikono na kukaa umbali wa zaidi ya mitaa moja na kuongeza kuwa hataruhusiwa mtu yeyote kuingia katika viwanja vyote vya mashindano ya kimichezo bila barakoa, vitakasa mikono na sabini ya kulipia

Nae msemaji wa Timu ya Maveterani jijini Mwanza ndugu Rajab Yahya amesema kuwa elimu ya kukabiliana na ugonjwa wa Covid-19 kwa wadau imetolewa katika muda muafaka na italeta tija katika kuhakikisha wanamchezo hawa walioathirika na ugonjwa huo, Wakati Ndugu Emanuel Seni Mratibu wa michezo ya UMITASHUMTA kanda ya Bugogwa akipongeza na kushukuru kwa elimu inayotolewa juu ya kujikinga na ugonjwa huo .
Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com