METDO Tanzania

METDO Tanzania

Saturday, June 27, 2020

DKT KALEMANI AFANYA ZIARA YA NYUMBA KWA NYUMBA KUKAGUA KAZI YA USAMBAZAJI UMEME VIJIJINI WILAYANI MISUNGWI

Waziri wa Nishati,Dkt Medard Kalemani(wa kwanza) akizungumza na Bi Restuta Willbad wakati alipokwenda kukagua nyumba ya mwanakijiji huyo wa kijiji cha Isamilo, Wilaya ya Misungwi,Mkoani Mwanza, Juni 26,2020
Waziri wa Nishati,Dkt Medard Kalemani, tarehe 26 Juni mwaka huu, amefanya ziara ya nyumba kwa nyumba ya ukaguzi wa kazi ya usambazaji umeme vijijini  katika Kijiji cha Usagara na Isamilo  wilayani Misungwi Mkoani Mwanza.
Katika ziara hiyo, iliyoanzia kwenye  kijiji cha Usagara na kumalizia ukaguzi huo katika kijiji cha Isamilo Dkt Kalemani aliweza kukagua zaidi ya nyumba 20 kwenye vijiji hivyo.
Akizungumza na wananchi wa kijiji cha Isamilo, alisema kuwa lengo la ziara yake ni kukagua  nyumba ambazo hazijaunganishwa na umeme katika kijiji hicho na   kujua sababu zilizofanya hadi sasa  hazina umeme, nyumba hizo ambazo zipo pembezoni mwa barabara.
“Sasa ndugu zangu wananchi nimekuja kwa kazi moja nimekuwa nikipita kwenye barabara hii mara kwa mara lakini kila nikitupa jicho mkono wa kushoto naona nyumba zenu zote hazina umeme jambo ambalo hatuwezi kulikubali” Alisema Dkt Kalema.
Alisema, mwanzoni mwa mwaka huu alitoa agizo nyumba hizo zianze kupelekewa umeme lakini mpaka sasa bado nyumba hizo hazina umeme.
Aidha, amelitaka Shirika la Umeme Tanzanai( TANESCO) ndani ya siku saba wawe tayari wamenza kuwapelekea umeme wananchi wa vijiji hivyo.
Pia, Dkt Kalemani ametoa agizo kwa Maafisa Uhusiano wa TANESCO nchni, kuwahamasisha wananchi kuweka umeme kwenye nyumba zao na kuwaeleza taaratibu za kuingiza kwenye nyumba zao, kuwambia wananchi majukumu yao na gharama za umeme.
Vile vile, amawataka wananchi wa vijiji  hivyo, kuanza mara moja kutafuta wataalamu wa kuwafanyia wiring kwenye nyumba zao ili wapelekewe umeme kwa haraka.
Aidha, amewataka wakandarasi nchini kufanya kazi kwa weledi na wasipofanya hivyo atawasimisha kazi mara moja na kuwapa kazi wakandarasi wenye uwezo.
“Mkoa wa Mwanza tulikuwa na mkandarasi tumefuta kazi na tumemuweka mkandarasi mwengine kwahiyo mkandarasi yoyote anaye legalega tutamfuta kazi na tumewapa  mpaka mwisho wa mwezi huu wawe wamemaliza kazi” Alisema.
Nae, Bi Restuta Willbad ambae ni mkazi wa kijiji cha Isamilo amesema kuwa,amefurahishwa na kitendo hicho cha Waziri cha kukagua nyumba zao na imewapa hamasa ya kwenda kulipia huduma ya umeme na wapo tayari kupokea huduma hiyo ambayo amesema itabadilisha Maisha yao kwa kuweza kujiajiri.
Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com