METDO Tanzania

METDO Tanzania

Monday, June 8, 2020

BARAZA LA MADIWANI HALMASHAURI YA WILAYA YA ARUSHA WA JADILI CHANGAMOTO YA MATUMIZI MABAYA YA FEDHA ZA TASAF

Na Agnes Geofrey

Halimashauri ya wilaya ya Arusha wamefanya kikao Cha baraza la robo tatu ya mwaka ikiwa na lengo la kujadili maendeleo ya miradi mbalimbali katika halimashauri hiyo.

Imeelezwa kuwa kumekua na Matumizi mabaya ya fedha za mfuko wa kusaidia kaya masikini (TASSAF) Katika maeneo mbali mbali ya halmashauri hiyo mikoani hapa ,Hali iliyosababisha kuwainua madiwani katika viti vyao kwenye Baraza hilo na kuomba taarifa za ukaguzi wa Matumizi ya fedha hizo. 

Akizungumza Katika Baraza hilo diwani wa viti maalum Yasmi Bachu amesema kuwa wataalamu wanaohusika na Mambo hayo Ni vyema kuingilia Kati na kuzikagua taarifa izo ili fedha na miradi inayotolewa iweze kuwafikia walengwa, kwani kumekuwa na Matumizi mabovu ya fedha hizo.

Bachu ameongeza kuwa Ni vizuri wataalamu wakachukua  changamoto na maoni ya baraza ili kuishauri serikali ni namba gani yakuwapata walengwa kabla ya Julai mwaka huu, kwani baadhi ya kaya zilizopo kwenye mradi huo hazikidhi vigezo ,badala yake watu maskini hawapati  fulsa huku kwaupande wa miradi ni nini kifanyike ili kuhakikisha fedha hazipotei lakini miradi inaleta tija.

Nae afisa mipango miji wa halimashauri hiyo Anastasia Tuhiba  amefafanua kwamba ubadilishwaji wa njia ya upokeaji wa fedha ndio umesababisha kuwepo kwa sintofahamu Katika suala zima la matumizi ya pesa hizo .

Sanjari na hayo Mwekekiti wa halimashauri hiyo, Baraka Simon ameiagiza TASSAFU  kuwa na muingiliano mzuri kwenye idara yenyewe pamoja na kamati husika kwenye miradi hiyo ili kuepusha migongano inayotokea, kwani miradi hiyo  inagharimu fedha nyingi ikiwa zaid ya billion 856.5 ,nakuwataka kuwa na ushirikiano kwanzia ngazi ya chini ya serikali ili kuweza kufanya kazi kwa uweledi mkubwa.
Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com