Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Dkt.Harrison Mwakyembe
akizungumza na uongozi wa Arusha Press Club
kuhusu namna bora ya kutekeleza majukumu yao kwa kuzingatia Sheria na kanuni za
Habari leo Jijini Dodoma.
Katibu Mkuu Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Dkt.Hassan Abbas
akizungumza katika kikao cha Waziri wa Wizara hiyo Dkt.Harrison Mwakyembe
(kushoto) pamoja na Uongozi wa Arusha Press Club kuhusu namna bora ya
kutekeleza majukumu yao ya kutoa habari sahihi kwa wananchi leo Jijini Dodoma.
Mwenyekiti wa Arusha Press Club Bw.Claud Gwandu akizungumza jambo wakati wa
kikao na Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Dkt.Harrison Mwakyembe
(kulia) ambapo walijadiliana masuala
mbalimbali yanaohusu tasnia ya
habari leo Jijini Dodoma.
Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Dkt.Harrison Mwakyembe
akipokea kipeperushi cha majukumu ya
Uongozi wa Arusha Press Club mara baada ya kumaliza kikao na Uongozi huo
kuhusu namna bora ya kutekeleza majukumu yao ya
kihabari leo Jijini Dodoma.
Wizara ya
Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo imezitaka ofisi za Umma kutoa taarifa kwa
wanahabari kwa kuwa siyo hisani na siyo hiyari, bali ni takwa la kisheria kwa
mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ibara ya 18 (d).
Kauli hiyo
imetolewa na Waziri mwenye dhamana ya tasnia ya Habari Dkt. Harrison Mwakyembe
alipokutana na ujumbe wa viongzi wa Chama cha Waandishi wa Habari kutoka mkoani
Arusha pamoja na Asasi ya Vyombo vya Habari Mbadala (Alternative Media) leo
jijini Dodoma.
“Serikali
haina ugomvi na vyombo vya habari, bila vyombo vya habari hatutaweza
kuwahabarisha wananachi masuala mbalimbali ya maendeleo ya nchi yetu” amesema
Dkt. Mwakyembe.
Aidha,
amewakumbusha wanahabari kuwa kazi wanayofanya ni muhimu sana ambapo nchi
zilizoendelea bado wanatumia vyombo vyao vya habari ikiwemo Shirika la
Utangazaji la Uingereza (BBC) ambalo lina miaka zaidi ya 90 na linatangaza
habari zake kwa lugha zaidi ya 40 ili kuwafikia wananchi wake na dunia kwa
ujumla.
Kwa upande
wake Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari kutoka mkoa wa Arusha Bw. Claud Gwandu amemshukuru Waziri
Dkt. Mwakyembe kwa mapokezi, majadiliano yenye tija kwa uwazi na ukweli na
kumpongeza kwa kazi nzuri anayofanya katika sekta anazozisimamia.
“Tunamshukuru
Waziri kwa kutupa nafasi ili tuweze kushirikiana katika kuimarisha tasnia ya
habari iwe bora kwa mustakabali wanchi yetu” amesema Gwandu.
Aidha,
Mwenyekiti huyo amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John
Pombe Magufuli kwa kazi kubwa anayofanya kwa kutekeleza miradi mingi kwa
manufaa ya Watanzania na kusisitiza kwa mwenye macho haambiwi tazama.
0 comments:
Post a Comment