Waziri wa
Madini Doto Biteko akisisitiza jambo wakati wa
Ufunguzi wa zoezi la Ugawaji fidia kwa wananchi wa Vijiji vya Matongo na
Nyabichune Wilayani Tarime mkoa wa Mara.![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEil_zYAoT58IgAfdQ18FUH77Nf2X1-G9eTw5hsZow_0ECD6JxbXRC6Fs8LnWkQ_6hlOKbVlbCh-AL48oPxlRWdJYHM8PO8NpAwUVsJNm7Eq5YMTuh3ziOV2uKa0Fxrz17bjgVTF98cebRmX/s1600/2+%25288%2529.jpg)
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEil_zYAoT58IgAfdQ18FUH77Nf2X1-G9eTw5hsZow_0ECD6JxbXRC6Fs8LnWkQ_6hlOKbVlbCh-AL48oPxlRWdJYHM8PO8NpAwUVsJNm7Eq5YMTuh3ziOV2uKa0Fxrz17bjgVTF98cebRmX/s1600/2+%25288%2529.jpg)
Waziri wa
Madini Doto Biteko akionesha jambo wakikagua bwawa la Kuhifadhi Tope Sumu (TFS)
katika Mgodi wa Barrick North Mara.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais
Muungano na Mazingira Mussa Azzan Zungu akizungumza jambo wakati wa zoezi la
Utoaji Fidia kwa wannchi wa eneo la Nyamongo
Naibu
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Angelina Mabula, akizungumza
jambo wakati wa utoaji Fidia kwa Wananchi wa Vijiji vya Matongo na Nyabichune
Wilayani Tarime mkoa wa Mara.
Hatimaye
Wakazi 1,639 wa Vijiji vya Matongo na Nyabichune katika eneo la
Nyamongo Wilayani Tarime Mkoa wa Mara wamelipwa fidia ya jumla ya Shilingi
Bilioni 33 baada ya kusubiri kwa kipindi cha miaka 10.
Fidia hiyo
imelipwa Mei 20, 2020 na Mgodi wa Barrick North Mara ikiwa
Utekelezaji wa Maagizo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John
Magufuli aliyoyatoa wakati wa ziara yake Mkoani humo ambapo alitaka suala hilo
ikiwemo la uchafuzi wa mazingira yamalizwe haraka.
Akizungumza
wakati wa Ufunguzi wa utoaji fidia na Ugawaji wa Cheki kwa Wakazi hao
waliopisha maeneo yao kwa ajili ya ajili ya uendelezaji wa shughuli za mgodi
huo, Waziri wa Madini Doto Biteko amewahakikishi wote wenye haki ya kulipwa
fidia hiyo kuwa watalipwa fedha zao.
Aidha,
ametoa pongeza kwa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi na
kueleza kuwa Wizara hiyo ilifanya kazi usiku na mchana kuhakikisha inamaliza
mgogoro wa fidia uliokuwepo baina ya wananchi na mgodi huo.
Pia,
amempongeza Mthamini Mkuu wa Serikali kwa kazi ya uthamini iliyofanyika
hatimaye kuwezesha wananchi wanaopaswa kulipwa fidia zao wanalipwa na
kuongeza, " maisha ya kutegesha yamekwisha, Serikali haitakubali
kushuhudia watengeneza migogoro wakitengeneza migogoro hapa".
Katika
hatua nyingine, ameiagiza Bodi ya Kampuni ya Twiga Corporation Limited
kuhakikisha inaufungaminisha Mgodi huo
na shughuli za Wananchi kiuchumi ili waweze kunufaika na uwepo wa Mgodi wake.
"
Tunataka Sekta ya Madini ifungamanishwe na sekta nyingine za kiuchumi, lakini
tunataka Wananchi wa Nyamongo wafanane na dhahabu inayochimbwa
hapa," amesisitiza Waziri Biteko.
Vilevile,
ameutaka Mgodi huo kuangalia na kuzifanyia kazi changamoto za kijamii
zinazowakabili wananchi wanaozunguka mgodi huo zikiwemo za maji, barabara
na ili kujenga mahusiano mazuri na jamii hiyo.
Kwa upande
wake, Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, Mussa Azzan
Zungu amesema Wizara yake imejiridhisha kuhusu Usalama wa taka Sumu na kuongeza
kuwa mara kwa mara umekuwa ukifanyika ukaguzi kuhakikisha maji hayo
hayaathiri wananchi wanaozunguka Mgodi huo. Pia, amewahakikishia Wananchi
kuhusu ufuatiliaji wa Sheria na taratibu za mazingira kuhusu suala hilo.
Akizunguzia
kuhusu matumizi ya zebaki, amewataka wachibaji nchini kuachana na matumizi ya
zebaki kwani madhara yake ni makubwa pindi inapoingi mwilini.
Naye, Naibu
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Angelina Mabula amesema zoezi
la utoaji fidia lilichukua muda mrefu kwasababu wananchi hawakuwa wakitoa
taarifa sahihi na baadhi kutegesha na
akatumia kutumia fursa hiyo kuwaasa wananchi
kutoa ushirikiano na kuwa wa
kweli kwenye masuala yote yanayohusu ulipaji fidia.
Kwa upande
wake, Meneja Mkuu wa Migodi ya Barrick Hilaire Diarra, amesema kampuni
hiyo imeanza safari Mpya ya Amani, ufanisi wa pamoja kwa Maendeleo ya Jamii.
Ameongeza kwamba, kwa miaka mingi mahusiano kati ya mgodi na jamii hiyo
yamekuwa siyo mazuri lakini hivi sasa
mgodi huo unaamini katika kuyajenga upya.
Ameongeza
kuwa Kamati ya Maendeleo ya Jamii imeundwa ili kuangalia vipaumbele katika eneo
hilo na yote yatafanyika kupitia Kamati hiyo.
"
Tumetembea miezi minne (4) kufikia hapa, makinikia, ushuru, utafiti, vibali vya
kazi, wafanyakazi wa nje, Usajili wa Jina la Twiga. Nakumbuka mara mwisho Mhe.
Waziri ulikuwa bado ukisisitiza suala la fidia liwe historia," amesema
Diarra.
Wakizungumza
katika Mahojiano Maalum na TBC ARIDHIO, Katibu Mkuu wa Madini Prof. Simon
Msanjila amesema suala hilo lilichukua muda mrefu hatimaye sasa Wananchi na
mgodi wamekubaliana, hivyo kupelekea kulipwa kwa fidia hiyo ya Shilingi Bilioni
33.
Naye,
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mary Makondo
amesema wananchi waliofanyiwa uthamini wamepata fidia ya haki.
Kwa upande
wake. Mkurugenzi Mkuu wa Baraza la Uhifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC)
Dkt. Samwel Gwamaka amesema Mamlaka hiyo inafanyia kazi malalamiko
ya wananchi wanaozunguka migodi Sambamba na kukagua iwapo taratibu za mazingira
zinafuatwa.
Ameongeza
kuwa Barrick North Mara ni miongoni mwa migodi inayofuatiliwa kuhakikisha
uendeshaji wake hauleti madhara kwa wananchi.
Katika hatua nyingine, Mkurugenzi wa wateja wa
Benki ya Benki ya CRDB, Boma Raballa, imeahidi kutoa huduma bora za kibenki kwa
wananchi waliolipwa fidia kwa kuhakikisha inatoa elimu kuhusu matumizi bora ya
fedha walizozipata ikiwemo kuhakikisha wanapata fedha hizo haraka.
Aidha,
mbali na kushuhudia ufunguzi wa utoaji fidia, Viongozi walioshiriki katika
zoezi hilo pia wametembelea na kukagua Bwawa la kuhifadhi Tope Sumu ( TFS)
katika Mgodi huo.
0 comments:
Post a Comment