Naibu Waziri wa Kilimo Mhe. Omary Mgumba
akimsikiliza Mkuu wa Kituo cha Utafiti TARI Hombolo Dkt. Lameck Makoye ndani ya
shamba la kuzalisha mbegu bora za mtama lenye ukubwa wa hekta 20
Naibu Waziri wa Kilimo Mhe. Omary Mgumba
akiangalia shamba la kuzalisha mbegu za uwele katika ziara yake ya kujionea
shughuli za uzalishaji wa mbegu katika Kituo cha TARI Hombolo leo
Naibu Waziri wa Kilimo Mhe. Omary Mgumba
akiangalia suke la ulezi kwenye shamba la kuzalisha mbegu bora katika ziara
yake ya kujionea shughuli za uzalishaji wa mbegu katika Kituo cha TARI Hombolo
leo
Naibu
Waziri Kilimo Mhe. Omary Mgumba amewapongeza Watafiti wa Kituo cha Utafiti
Hombolo (TARI – Hombolo) kwa kuanza kutekeleza kwa vitendo agizo la kuongeza
uzalishaji wa ndani wa mbegu bora za mazao ya jamii ya nafaka zinazovumilia
mvua kidogo kama ulezi, uwele na mtama.
Naibu
Waziri Mgumba ameyasema hayo mapema leo tarehe 17 Mei, 2020 mara baada ya
kutembelea Kituo cha Utafiti Hombolo ili kujionea maendeleo ya utafiti wa mazao
ya kilimo pamoja na ufikishaji wa teknolojia mbalimbali zilizogunduliwa na
Watafiti kwenda kwa Wakulima.
Mhe. Mgumba
amesema amefurahi kuona TARI Hombolo imeanza kutekeleza lengo la Serikali la
kujitosheleza kwa mbegu bora na kupunguza uagizaji wa mbegu bora kutoka nje ya
nchi.
Mhe. Mgumba
amesema katika kipindi hiki cha miaka minne ya Serikali ya Awamu ya Tano
upatikanaji wa mbegu bora umeongezeka kutoka tani 36,614 mwaka 2015/2016 hadi
tani 76,725 mwaka 2019/2020 sawa na ongezeko la asilimia 110.
“Uzalishaji
wa ndani wa mbegu bora, umeongezeka kutoka tani 20,604 mwaka 2015/2016 hadi
tani 69,173 mwaka 2019/2020. Uzalishaji huo umepunguza uagizaji wa mbegu bora
kutoka nje ya nchi kutoka tani 16,009 mwaka 2015/2016 hadi tani 7,552 mwaka
2019/2020 sawa na punguzo la asilimia 53. Amekaririwa Mhe. Naibu Waziri Mgumba.
Naye Mkuu
wa Kituo cha TARI Hombolo Dkt. Lameck Makoye amesema malengo makuu ya Kituo
hicho ni kufanya utafiti, kusambaza teknolojia kwa njia mbalimbali na kuzalisha
mbegu za mazao yanayovulia mvua za wastani kama ulezi, uwele na mtama.
Dkt. Makoye
ameongeza kuwa Kituo cha TARI Hombolo kwa kushirikiana na Taasisi ya ICRISAT
wamefanikiwa kufanya utafit za zao la mtama na kupata mbegu bora ‘Hybrid’ 36.
Aidha TARI
Hombolo kwa kushirikina na Kampuni ya Advantha Seed International imefanikiwa
kufanya utafiti kwa mazao ya ulezi, uwele na mtama maalum kwa ajili ya malisho
ya mifugo kama ng’ombe, mbuzi na kondoo na kuja na mbegu bora kama Sugar Graze,
Mega Sweet, BMR Rocket, Jumbo Rocket na Nutrified.
Naibu
Waziri Mgumba ameagiza pia kwa Taasisi hiyo kuendelea kujikita katika Miradi
mikubwa ambayo italeta tija kwa Taasisi; Ukiwemo Mradi wa kuzalisha mbegu za
mtama aina ya MACIA ambayo inasoko kubwa kwa ajili ya kutengeneza ‘beer’ aina
ya IGO ambapo Wakulima wengi wamepata soko la uhakika kutoka Kiwanda cha Bia
cha TBL.
Watumishi
wa TARI Hombolo wamemueleza Naibu Waziri Mgumba kuwa kuna changamoto kadhaa
ambazo zinahitaji utatuzi ili Taasisi ijiendeshe kwa tija, moja ya chamaoto
hizo ni majengo kwa ajili ya kuhifadhi mbegu bora, eneo kubwa la kuzalishia
mbegu, maeneo ya kilimo ya Kituo kuvamiwa pamoja na vitendea kazi kama matrekta
madogo na makubwa ajili ya kulima eneo kubwa na kuvuna kwa kutumia zana bora.
Naibu
Waziri Mgumba aliahidi kushughulikia changamoto zote hizo kwa kushirikiana na
Viongozi wengine wa Wizara ya Kilimo.
0 comments:
Post a Comment