Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe akizungumza leo Jijini Dodoma na Waandishi
wa Habari kuhusu mfumo utakaotumika katika michezo ya ligi inayotarajiwa kuanza June mosi, 2020 ambapo ameeleza
Michezo hiyo ni Ligi Kuu, ligi daraja la kwanza, daraja la pili na na kombe la
shirikisho la Azam huku akieleza viwanja vitakavyumika kuwa ni vya Jijini Dar
es Salaam na Mwanza
Serikali
imeruhusu ligi kuu nne kuanza kuchezwa nchini kuanzia Juni 1, 2020 kwa
tahadhari zote ili kumpata bingwa wa ligi hizo na timu mwakilishi katika Kombe
la Shirikisho Barani Afrika.
Kauli hiyo
imetolewa na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison
Mwakyembe katika mkutano na waandishi wa habari leo jijini Dodoma kuhusu uamuzi
wa Serikali wa kuanza kwa ligi hizo baada ya kusitishwa kwa muda kufuatia
ugonjwa mlipuko waugonjwa wa homa kali
ya mapafu (COVID-19) unaosababishwa na virusi vya Corona.
“Tunaruhusu
ligi nne tu kwa kuanzia hali ikiendelea
vizuri tunafungulia michezo yote, kwasasa tunafungulia ligi kuu, ligi
daraja la kwanza, ligi daraja la pili na kombe la shirikisho la Azam” amesema
Dkt. Mwakyembe.
Ili ligi
hizo ziweze kuchezwa kwa ufanisi, Dkt Mwakyembe amesema zitachezwa katika vituo
vikuu viwili ambavyo ni Dar es salaa na Mwanza ambapo kwa upande wa kituo cha
Dar es Salaam uwanja vya Taifa, Uhuru na Chamazi na kituo cha Mwanza viwanja
vitakavyotumika ni CCM Kirumba na Nyamagana.
Waziri Dkt.
Mwakyembe amesema kituo cha Dar es Salaam kitahusisha mechi za ligi kuu pamoja
na kombe la shirikisho la Azam wakati
kituo cha Mwanza kitahusisha ligi daraja la kwanza na ligi daraja la pili.
Dkt.
Mwakyembe ameongeza kuwa Katibu Mkuu wa wizara hiyo Dkt. Hassan Abassi kuanzia
jana ameruhusu wachezaji wa vilabu hivyo waanze kufanya mazoezi ili kujiandaa
na michezo hiyo kwa kuwa wamekaa muda mrefu tangu michezo kusitishwa mapema
mwezi Machi 2020.
Aidha, Dkt.
Mwakyembe amezihimiza taasisi zinazohusika na utaalamu zihakikishe ratiba ya
michezo hiyo inatolewa mapema ili ili mashindano hayo yafanyike kwa ufanisi.
Taasisi
zinazosimamia mashindano hayo ni Shirikisho la Mpira wa Miguu (TFF), Bodi ya
ligi, Baraza la michezo la Taifa (BMT), Kurugenzi ya Maendeleo ya Michezo
pamoja na wasimamizi wa viwanja.
Vile vile
Waziri huyo ameongeza kuwa Serikali imeweka utaratibu ambao unazidi kuboreshwa
ambapo wachezaji wote watapimwa joto, na
kutahadharisha upimaji huo usiwe na vitu vya kuhujumu timu na wachezaji hivyo
ameiagiza BMT kushirikiana na Wataalam wa Afya katika zoezi hilo.
0 comments:
Post a Comment