Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani( pili
kulia) aliyeambatana na Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya TANESCO, akipita kukagua
shughuli za ujenzi wa upanuzi wa kituo cha kupoza na kusambaza umeme cha Zuzu
jijini Dodoma, Aprili, 30,2020, katikati ni Naibu Waziri wa Nishati Subira
Mgalu.
Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani(,(
mwenye kofia nyeupe) akiwa na Wajumbe Bodi ya Wakurugenzi ya TANESCO)
akimueleza jambo Mwenyekiti wa bodi hiyo, Dkt, Alexander Kiyarunzi (kushoto)
walipotembelea eneo la kuhifadhi nguzo wakati wa ziara ya kukagua ujenzi wa
upanuzi wa kituo cha kupoza na kufua umeme cha Zuzu jijini Dodoma, Aprili
30,2020.
Vijana wakiendelea na kazi ya ujenzi katika
kituo cha kupoza na kusambaza na umeme cha Zuzu jijini Dodoma, wakati wa ziara
ya Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani na Wajumbe wa Bodi ya wakurugenzi ya
TANESCO ya kukagua ujenzi wa upanuzi wa
kituo hicho Aprili 30,2020.
Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani
(katikati) pamoja na Wajumbe wa Bodi ya wakurugenzi ya TANESCO wakipata maelezo kutoka kwa msimamizi mkuu wa
kituo cha kupoza na kusambaza umeme cha Zuzu jijini Dodoma, baada ya kufanya
ziara ya kukagua ujenzi wa upanuzi wa kituo hicho, Aprili 30,2020.
Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani(
katikati) akizungumza na Wajumbe wa Bodi ya wakurugenzi ya TANESCO wakati wa
kikao baada ya ziara ya kukukagua ujenzi wa upanuzi wa kituo cha kupoza na
kusambaza umeme cha Zuzu jijini Dodoma, Aprili 30,2020, kulia ni Naibu Waziri
wa Nishati, Subira Mgalu na kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati,
Mhandisi Zena Said.
Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya TANESCO
wakimsilikiza Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani,( hayupo pichani) wakati
wa kikao baada ya ziara ya kukukagua ujenzi wa upanuzi wa kituo cha kupoza na
kusambaza umeme cha Zuzu jijini Dodoma,Aprili 30,2020.
Waziri wa
Nishati Dkt. Medard Kalemani ameliagiza Shirika la Umeme nchini( TANESCO)
kuendelea kukata umeme kwa wadaiwa sugu ili kukusanya mapato zaidi na kulipa
madeni ya shirika hilo.
Dkt.
Kalemani alisema hayo, Aprili 30, 2020, Jijini Dodoma, alipokutana na Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa TANESCO,
kuzungumzia tathimini ya miaka mitano ya utekelezaji wa miradi mbalimbali,
baada ya kufanya ziara ya kukagua ujenzi wa upanuzi wa kutuo cha kupoza na
kuzambaza umeme cha Zuzu.
Katika kikao
hicho, mambo mbalimbali yalijadiliwa kuhusiana na nishati ya umeme
inayozalishwa nchini kwa lengo la kuleta manufaa makubwa zaidi kiuchumi kwa
nchi, Shirika na watumiaji wa umeme huo ikiwemo viwanda, wafanyabiashara na
matumizi mengine.
Dkt.
Kalemani aliiagiza TANESCO, kulipa madeni yote inayodaiwa na kutoongeza madeni
mapya, vilevile wadaiwa sugu wakumbushwe madeni yao,na endapo hatawalipa,
TANESCO iwakatie umeme, kwa kufanya hivyo kutamaliza tatizo la wadaiwa sugu.
“TANESCO
inadaiwa madeni makubwa, pia ina wateja wengi sana ambao ni wadaiwa sugu
wanaodaiwa fedha nyingi sana na hawalipi ,zimo Taasisi, Mashirika ya Umma na
binafsi, pamoja na watumiaji wa kawaida, ninawaagiza nendeni mkawakatie umeme!
narudia tena mkakate umeme! mkishaukata, wahusika watalipa na wataonyesha
ushirikiano mkubwa, tofauti na kumdai kawaida tu”, alisema Dkt. Kalemani.
Kuhusu wizi
na uhujumu wa miundombinu ya umeme, Dkt. Kalemani, aliitaka TANESCO, Bodi ya
TANESCO na Watendaji wa Wizara ya Nishati, kushirikiana kwa pamoja kutafuta
njia sahihi naya kisasa zaidi ya kubaini
wizi wa umeme,unaofanywa na watu wasiowaaminifu na kusababisha hasara kwa
shirika na kupoteza mapato ya taifa.
“Wizi wa
umeme upo na haukubaliki, tuweke mfumo sahihi wa kisasa kubaini wahusika,
tuache na hii tabia ya kukimbizana kimbizana na wezi, pia sisi watumishi tuwe
wazalendo,na wasimamizi wazuri wa miundombinu yetu,vilevile tuwe na walinzi
wenye weledi katika miradi yetu bila kujali niya serikali au mtu binafsi,
jukumu la ulinzi ni letu sote faida ya Taifa kwa jumla”,alisisitiza Dkt.
Kalemani.
Aidha
aliwataka kuendelea kufanya tathmini na uwiano wa gharama za kutengeneza nguzo
za Zege na nguzo zinazotumika sasa,ili kuangalia uwezekano wa kutumia nguzo za
zege katika maeneo yote nchini lakini kwa gharama nafuu, kwa lengo la
kukabiliana na changamoto ya kuoza ama kuungua kwa nguzo katika maeneo
mbalimbali.
Hata hivyo
aliweka wazi kuwa katika baadhi ya maeneo machache ambayo ni korofi nguzo za
zege zimeanza kutumika japo ni za gharama kubwa.
Vilevile
alitaka kuongezeka kwa idadi ya wateja wa umeme katika kila sekta, kuharakisha
uunganishaji wa umeme kwa mteja pale anapomaliza kulipia gharama husika, pamoja
na kutatua changamoto za wateja kwa wakati sahihi ili kuvutia wateja wengi
zaidi na kuondoa malalaliko.
Kwa upande
wake, Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu aliwataka TANESCO kuangalia
uwezekano wa kutoa zawadi kubwa kwa wasamaria wema wanaotoa taarifa za siri
kuhusu wanaohujumu na kuiba umeme tofauti na ile inayotolewa sasa, ambayo pia
huchukuwa muda mrefu kuikabidhi kwa mhusika.
Mgalu
alikitaka kitengo husika kitunza siri za
watoa taarifa,pia kifanye uchunguzi wa kina na kutoa adhabu kwa mtumishi yeyote
atakayetiliwa shaka, au kuhusika na wizi pamoja na kuhujumu miundombinu ya
umeme kama inavyofanywa kwa wahisika wengine wanaobainika.
Vilevile
kuwe na uhamasishaji wa kuwavutia watoa taarifa ili kupata matokeo chanya
kunusu wizi na uhujumu wa miundombinu ya umeme nchini.
Naye Katibu
Mkuu wa Wizara hiyo, Mhandisi Zena Said, alieleza kuwa ili kukabiliana na changamoto
ya wizi na uhujumu wa miundombinu ya umeme, watashirikiana na Ofisi ya Rais,
Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa,(TAMISEMI) kuimarisha ulinzi kuanzia ngazi
za Kaya.
Mhandisi
Said, alisema kwa kufanya hivyo kutasaidia sana kubaini wezi na wahujumu miundombinu
ya umeme kwa kuwa watu hao wasio wazalendo huwa wanaoneka na hata kufahamika
katika maeneo yao.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa TANESCO, Dkt. Alexander Kyaruzi, aliishuruku
Wizara ya Nishati kwa kuwapa ushirikiano mkubwa katika kutekeleza majukumu yao
na kuyafanyia kazi yale waliokuwa wakiishauri wizara hiyo, katika kipindi chote
cha miaka mitano
Dkt.Kiyarunzi,
alikiri kwa kuwa kazi ya kusambaza umeme si jambo jepesi, hivyo wanajivunia
kuona maendeleo makubwa katika sekta ya nishati ya kuongeza wigo wa usambazaji
wa umeme vijijini, kujenga miradi mikubwa ya kuzalisha, njia za kusafirisha na
kusambaza umeme pamoja na vituo vya kupoza na kusambaza umeme nchini.
Awali kabla
ya kufanyika kwa kikao hicho, Uongozi wa Wizara na Wajumbe wa Bodi hiyo walifanya
ziara ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa upanuzi wa Kituo kikubwa zaidi nchini
cha Kupoza na kusambaza umeme cha Zuzu kilichopo jijini Dodoma.
Kwa mujibu
wa Dkt. Kalemani, ujenzi wa kituo hicho utakamilika mwishoni mwa mwezi huu wa
Mei, 2020 na kitakuwa na uwezo wa kuzalisha Megawati 648 tofauti na vituo
vingine.
Na kituo
hicho kitaimarisha upatikanaji wa umeme kwa Jijiji la Dodoma ambalo linaendelea
kukuwa kwa kasi na kitakuwa ndiyo kitovu
cha vituo vyote vya kupoza kuzambaza umeme katika mikoa yote nchini na
kuupeleka nchi jirani pale itakapohitajika kufanya hivyo.
0 comments:
Post a Comment