Waziri wa
Nishati, Dkt. Medard Kalemani ( kulia) akiwasha umeme katika Kijiji cha Bugwego Kata ya Bwongera, wilayani
Chato mkoani Geita alipofanya ziara ya kukagua maendeleo ya usambazaji umeme
vijijini katika maeneo hayo, Mei 18,2020.
Waziri wa
Nishati, Dkt. Medard Kalemani(kushoto),akizungumza na mmoja wa wakazi wa Kijiji
cha Rusungwa Kata ya Nyamirembe,Wilayani Chato,mkoani Geita baada ya kuwasha
umeme katika nyumba yake alipofanya ziara ya kukagua maendeleo ya usambazaji
umeme vijijini katika maeneo hayo, Mei 18,2020.
Waziri wa
Nishati, Dkt. Medard Kalemani,( kushoto) akiruka maji wakati akienda kukagua
maendeleo ya usambazaji wa umeme vijijini katika Kijiji cha Bugwego Kata ya
Bwongera Wilayani Chato,mkoani Geita, alipofanya ziara ya kukagua maendeleo ya
usambazaji umeme vijijini katika maeneo hayo, Mei 18,2020. Dkt. Kalemani
alilazimika kutembea kwa mguu kufikia maeneo hayo kuwa magari hayafiki kwa
sababu ya kuharibika kwa barabara kufuatia mvua kubwa zilizokuwa zinanyesha
katika maeneo mbalimbali nchini.
Waziri wa
Nishati, Dkt. Medard Kalemani ( katikati) akiwasha umeme katika Kata ya Businda wilayani Bukombe mkoani Geita
alipofanya ziara ya kukagua maendeleo ya usambazaji umeme vijijini katika
maeneo hayo, Mei 18,2020.
Waziri wa
Nishati, Dkt. Medard Kalemani ( kulia) akizungumza na wakazi wa Kata ya Businda
wilayani Bukombe mkoani Geita(hawapo pichani) alipofanya ziara ya kukagua
maendeleo ya usambazaji umeme vijijini katika maeneo hayo, Mei 18,2020.
Waziri wa
Nishati, Dkt. Medard Kalemani amewaambia wanakijiji ambao umeme ushafika katika
maeneo yao walipie gharama za kuwashiwa umeme ili kufahamu idadi ya wateja,
nguzo zisambazwe na kuunganishwa kulingana na wateja waliopo kwa wakati husika.
Dkt.
Kalemani alisema hayo wakati akiwasha umeme katika Kijiji cha Rusungwa Kata ya
Nyamirembe, Bugwego Kata ya Bwongera Wilayani Chato na Kijiji cha Businda
Wilayani Bukombe mkoani Geita alipofanya ziara ya kukagua maendeleo ya
usambazaji umeme vijijini katika maeneo hayo, Mei 18,2020.
Dkt. Kalemani
alisema kuwa vijiji vingi tayari vimefikiwa na umeme katika maeneo machache
hivyo wananchi wanatakiwa kulipia gharama za kuwashiwa umeme ili ifahamike
idadi ya wateja waliopo na kupelekewa nguzo za kusambazwa kwa wateja waliopo na
wawashiwe umeme.
Pia
alieleza kuwa kitendo cha wanakijiji kuacha kulipia gharama za kuuwashiwa umeme
wakisubiri kuona nguzo zimesambaa katika maeneo yao, hali ya kuwa tayari umeme
umeshafika katika vijiji vyao, kunachelewesha kasi ya kuwawashia umeme
wanakijiji katika nyumba zao kwa kuwa mamlaka husika zinasambaza nguzo
kulingana na wateja waliopo eneo husika kwa wakati husika, hivyo wananchi
wachangamkie fursa na kulipia gharama ya shilingi 27,000 tu.
Vilevile
alisema kuwa wanakijiji hao hawapaswi kuhoji kuhusu nguzo kufika katika maeneo
yao kwakuwa hilo si jukumu lao, ila wanachotakiwa kufanya ni kulipia gharama za
kuwashiwa umeme tu, na baada ya kulipia gharama ndipo wahoji endapo
hawajawashiwa umeme.
"Kijiji
chochote ambacho umeme umeshafika na kuunganishwa, hata kama umewashwa katika
nyumba moja, wanakijiji sasa jukumu lenu ni kulipia gharama kuwashiwa umeme ili
ijulikane idadi ya wateja waliopo na mletewe nguzo na kuungwa, nguzo zinaletwa
na kusambazwa kulingana na idadi ya wateja waliopo,kwa wakati husika ili wote
wanaotaka kwa wakati huo wapate, msihoji kuwa nguzo zinafika lini hilo si
jukumu lenu! Ninyi mnapaswa kuhoji lini mtawashiwa umeme mkiwa tayari mmelipia
gharama, na hapo tutachukua hatua kwa yeyote atakayechelewa kumuwashia umeme
mteja aliyekwisha lipia gharama za uunganishaji, Sasa lipieni msisubiri nguzo
”, Alisema Dkt. Kalemani
Aidha Dkt.
Kalemani alirejea kusema kuwa mkandarasi yeyote atakayeshindwa kumaliza kazi ya
usambazaji wa umeme vijijini kwa mujibu wa mkataba,atashitakiwa kisheria kwa
kosa la kuwacheleweshea wananchi huduma pamoja na kukatwa asilimia 10 ya malipo
yake yaliyosalia.
Aidha kazi
hiyo atapewa mkandarasi mwingine amalizie na hiyo asilimia 10 iliyokatwa ndiyo
itatumika kumlipa mkandarsi atakayekabidhiwa jukumu la kumalizia kazi hiyo.
Aliendelea
kuwasisitiza wakandarasi walio nyuma ya muda katika kukamisha kazi hizo kuongea
nguvu kazi katika maeneo ya kazi ili wasikumbane na kadhia hivyo.
Vilevile
alitoa wiki moja kwa mkandarasi kwa kushirikiana na Shirika la Umeme Tanzania(
TANESCO) kuwawashia umeme wakazi wa Mtaa
wa Businda waliokwisha lipia gharama hizo na kukumuagiza Mkuu wa Wilaya ya Bukombe kumchukulia hatua
mkandarasi wa eneo hilo endapo atashindwa kufanya hivyo.
Dkt.Kalemani
alisema kuwa mkandarasi yeyote ambaye hakufanya vizuri katika utekelezaji wa
mradi wa usambazaji wa umeme vijijini (REA), hatapewa nafasi ya kufanya kazi
katika miradi inayokuja hata kama ameshinda vigezo vya Zabuni.
"Mkuu
wa Wilaya nakukabidhi mkandarasi huyu akishindwa kuwauwashia umeme wanakijiji
hao waliolipia gharama pamoja na
kuwaunganishia wale aliowapita pale, mchukulie hatua ikiwezekana muweke
korokoroni, hii iwe fundisho kwa wakandarasi wengine nchini kwa sababu wengi
wanachewa kuwawashia wananchi umeme wakati tayati wamelipia, na utaratibu ni ndani
ya siku saba baada ya mwananchi kulipia awashiwe umeme sio kuwaacha tu bila
kuwaeleza sababu yoyote", Alisisitiza Dkt. Kalemani.
Pia
aliwawasisitiza mameneja wa TANESCO kote nchini kufanya kazi kwa bidii ili
kutimiza azma ya serikali ya kuunganisha umeme katika kijiji vyote nchini
ifikapo 2021, pia wazingatie viwango na tathmini iliyowekwa katika kuwapima
utendaji kazi wao.
Juni 30,
2020 wakandarasi wote nchini wanaotekeleza mradi wa usambazaji wa umeme
vijijini wanatakiwa kukamilisha kazi hiyo kwa mujibu wa mkataba, hata hivyo
serikali imekaririwa ikisemakuwa haitaongeza muda kwa yeyote ambaye atashindwa
kukamilisha kazi hiyo na tachukuliwa hatua kwa mujibu wa sheria.
0 comments:
Post a Comment