Mkuu wa
Chuo cha Maendeleo ya Michezo Malya Bw.Richard Mganga.
Hayo
yamesemwa na Mkuu wa Chuo hicho Bw.Richard Mganga katika mahojiano maalum
ambapo ameeleza kuwa watalaam waliozalishwa wametokana na kozi zitolewazo
chuoni hapo ambazo ni pamoja na; Michezo kwa ngazi ya Astashahada (Diploma)
katika fani ya ualimu wa Michezo (Coaching),Uongozi wa Michezo (Sports
Administration) pamoja na Usimamizi wa Michezo (Sports Management) lengo ikiwa
ni kuandaa watalam wazuri wa kukuza na kuendeleza michezo nchini.
“Chuo hiki kina utaratibu wa kutoa mafunzo nje
ya chuo pamoja na jamiii inayozunguka chuo hichi ambapo tangu kimeanzishwa kimekua
na utaratibu wa kutoa mafunzo ya muda mfupi kwa halmashauri mbalimbali nchini
na mwamko umekua mkubwa wa wadau kujifunza michezo”alisema Bw.Mganga.
Aliongeza
kuwa Chuo hicho ndicho pekee kinachotoa kozi za michezo hapa nchini kikilenga
kukuza sekta hiyo kwa kuzalisha wataalamu wenye sifa na viwango vya kimataifa.
Bw.Mganga
amezitaja Halmashauri ambazo zimenufaika na Chuo hicho kupitia mafunzo yaliyotolewa kuwa ni pamoja na
Halmashauri ya Wanging’ombe ya Mkoa wa Njombe,Kalambo Mkoani Rukwa,Iramba ya Mkoani
Singida,Iringa Mjini pamoja na Mpwapwa ya Mkoani Dodoma.
Kwa upande
wake, Mwalimu wa Chuo Hicho Bw.Mohamed Mwiduchi amesema kuwa, Chuo hicho kina
viwanja vizuri ambavyo jamii inayozunguka imekua na utaratibu wa kutumia katika
michezo, huku akieleza kuwa timu ambazo zimekua zikitumia waalimu wa chuo hicho
zimekua zikifanya vizuri katika mashindano mbalimbali.
Bw.Mwiduchi
ameongeza kuwa Chuo hicho kinafundisha michezo ya Mpira wa Pete,Mpira wa
Mikono, Mpira wa Kikapu na Mpira wa Wavu.
Chuo cha
Maendeleo ya Michezo Malya kipo katika Wilaya ya Kwimba Jijini Mwanza.
0 comments:
Post a Comment