METDO Tanzania

METDO Tanzania

Saturday, May 23, 2020

BODI YA CHAMA KIKUU CHA USHIRIKA RUKWA YATAKIWA KURUDISHA HESHIMU KWA WAKULIMA

Baadhi ya Wajumbe wa Bodi ya Chama Kikuu Cha Ushirika Mkoa ni Rukwa, Ufipa Co-operative  Union (UCU) wakisikiliza kwa makini nasaha za Katibu Tawala wa Mkoa (hayupo pichani)

Mrajis Msaidizi mkoa wa rukwa Benjamin Mangwala akitoa maneno ya utangulizi kabla ya mgeni rasmi Katibu Tawala wa Mkoa.

Katibu Tawala wa Mkoa wa Rukwa Benard Makali. 


Katibu Tawala wa mkoa wa Rukwa Benard Makali amewataka wajumbe wa Bodi ya Mpito ya Chama Kikuu cha Ushirika Mkoani Rukwa Ufipa Co-operative Union (UCU) kuhakikisha wanazingatia matakwa yote ya kisheria na miongozo ya usimamizi wa Chama hicho kwa weledi wa hali ua juu ili kurudisha heshimu ya Ushirika kwa wakulima na wananchi wa mkoa wa Rukwa.

Amesema kuwa utendaji kazi bora wa bodi hiyo utainua kipato cha wakulima ndani ya mkoa, na hatimae kuinua pato la taifa katika kukuza zao la mahindi na ufuta kwa wakulima hao kuuza kwa bei watakayoridhika nayo kupitia chama hicho na hivyo kuepukana na madalali wanaowafuata mkulima mmoja mmoja na kuwalaghai hali ambayo inawakandamiza na kurudisha nyuma maendeleo ya wakulima.

“Naamini ninyi viongozi wangu hapa mnaonitazama, ninajua kabisa kwamba mtasimama vizuri ili tuondokane na hizi kero ndogo ndogo, wengine saa hizi unakuta fuso limeshaingia shambani, mtu anapukuchua mahindi anauzia huko huko, ana shida, lakini pia licha ya shida hana pa kuweka, nyumbani zetu tunazijua yaani una watoto 10 halafu una gunia 300 utaziweka wapi, lakini kama tukiwa na ‘storage system’ nzuri ambayo iko ‘recorded’ vizuri, kwanza tutakuwa na heshimu, bei itakuwa nzuri, halafu watu watabadilika,” Alisema.

Ndugu Makali ameyasema hayo wakati alipofungua kikao kazi cha kupitia mwongozo wa masoko ya mazao ya wakulima wa zao la ufuta na mahindi kupitia vyama vya ushirika mkoa wa Rukwa kilicholenga kuwajengea uwezo wajumbe wa bodi ya mpito ya UCU juu ya namna bora ya kuwajibika katika usimamizi  wa Ushirika na hatua stahiki ya kuchukuliwa pindi wanapokutana na changamoto.

Awali akitoa ufafanuzi wa mwongozo huo Mrajis Msaidizi Mkoa wa Rukwa Benjamin Mangwala alisema kuwa mwongozo huo umebainisha majukumu ya kila mdau katika myororo wa thamani, kuanzia ngazi ya mkulima, msafirishaji, mnunuajia pamoja na nafasi ya halmashauri katika kupata mapato yake na kuongeza kuwa mwongozo huo unamtaka kila mkulima kuwa na akaunti yake benki ili aweze kulipwa moja kwa moja kutoka chama kikuu.

“Kwahiyo huu Mwongozo umeainisha maeneo yote, na pale ambapo mtu atakuwa amebainika, amekiuka, kwa maana ya kwamba atakuwa na mazao amebeba, amenunua kwa wakulima anataka asafirishe akakamatwa, pia mwongozo umeainisha kwamba ni adhabu ipi inayotakiwa itolewe na mamlaka ipi inatakiwa itoe hiyo adhabu,” Alisisitiza.

Katika kuhakikisha jambo hilo linafanikiwa tayari Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula nchini (NFRA) wameshirikishwa kwenye utaratibu wa mwongozo huo pamoja na kukaa vikao na mabenki ili kuwashawishi wakulima kuwa na akaunti zao.

Hatua hizi zimekuja baada ya kuvunjwa kwa iliyokuwa bodi ya UCU kuvunjwa mwezi March mwaka huu baada ya kutokea ukiukwaji wa taratibu za manunuzi ya mbolea kwa wakulima hali iliyopelekea wakulima hao kukwama kuhudumia mazao yao na hivyo kukosa Imani na chama hicho.
Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com