METDO Tanzania

METDO Tanzania

Wednesday, April 1, 2020

WAZIRI WA KILIMO NA WAZIRI WA VIWANDA WAONGOZA KIKAO KAZI KUJADILI UFUNGAMANISHAJI WA SEKTA YA KILIMO NA MIKAKATI YA KUTAFUTA MASOKO

Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Kushoto) na Waziri wa Viwanda na Bishara Mhe Innocent Bashungwa (Kulia) wakifuatilia hoja za washiriki wa kikao kazi cha kujadili namna ya kufungamanisha uchumi wa Kilimo na Viwanda Jijini Dodoma, leo tarehe 1 Aprili 2020. (Picha Zote Na Eliud Rwechungura, Wizara ya Viwanda na Biashara)
Sehemu ya wataalamu kutoka Wizara ya Kilimo na Wizara ya Viwanda na Biashara pamoja na AGRA wakifuatilia hoja za washiriki wa kikao kazi cha kujadili namna ya kufungamanisha uchumi wa Kilimo na Viwanda Jijini Dodoma, leo tarehe 1 Aprili 2020.
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akisisitiza jambo wakati wa kikao kazi cha kujadili namna ya kufungamanisha uchumi wa Kilimo na Viwanda Jijini Dodoma, leo tarehe 1 Aprili 2020.
Waziri wa Viwanda na Bishara Mhe Innocent Bashungwa (Kulia) akisisitiza jambo wakati wa kikao kazi cha kujadili namna ya kufungamanisha uchumi wa Kilimo na Viwanda Jijini Dodoma, leo tarehe 1 Aprili 2020.
Mshauri wa masuala ya Maendeleo ya Viwanda vya Kilimo wa Taasisi ya kuendeleza Kilimo Afrika (AGRA) Ndg Peniel Lyimo akichangia mada wakati wa kikao kazi kilichoongozwa na Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga na Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe Innocent Bashungwa cha kujadili namna ya kufungamanisha uchumi wa Kilimo na Viwanda Jijini Dodoma, leo tarehe 1 Aprili 2020.

Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Dodoma 

Wataalamu kutoka Wizara ya Kilimo kadhalika, Wizara ya Viwanda na Bishara, na Taasisi za soko la Bidhaa Tanzania (TMX), Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) na Taasisi ya kuendeleza Kilimo Afrika (AGRA) wamekutana Jijini Dodoma kujadili kwa pamoja namna ambavyo Wizara hizo mbili zinaweza kuongeza mshikamano na weledi wa kiutendaji kwa ajili ya kufungamanisha uchumi wa Kilimo na Viwanda.

Katika kikao hicho kilichotuama katika ukumbi wa Wizara ya Kilimo maarufu kama Kilimo IV kikiongoza na mawaziri kutoka pande mbili, Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) na Waziri wa Viwanda na Bishara Mhe Innocent Bashungwa (Mb) kwa pamoja wamesisitiza ulazima wa wataalamu hao kuunganisha nguvu kwa pamoja baina ya Wizara na Taasisi za umma na binafsi ili kuimarisha upatikanaji wa takwimu sahihi kuhusu Uzalishaji, uhifadhi, Ubora kwa Mazao ya kimkakati na mchanganyiko.

Akizungumza katika kikao hicho Waziri wa Kilimo Mhe Japhet hasunga (Mb) amewataka Wataalamu hao kuimarisha intelijensia ya masoko kwa kutumia mbinu mbalimbali ikiwemo na ufuatiliaji wa karibu wa mwenendo wa masoko ya Mazao na bidhaa ulimwenguni.

Hasunga amesema kuwa  pamoja na mikakati ya masoko lakini wataalamu hao wanaweza kujadili na kuona namna ya kuimarisha uhifadhi wa Mazao ya wakulima baada ya kuvuna kwani Barani Afrika nafaka myingi hupotea mara baada ya kuvuna.

Amewataka wataalamu hao pamoja na mambo mengine amewataka kuhakikisha kuwa wanaimarisha miundombinu ya masoko ikiwemo maghala ya kisasa ya kuhifadhia Mazao na bidhaa.

Naye, Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe Innocent Bashungwa (Mb) amesema kuwa intelijensia ya masoko inapaswa kuhakikisha kwa haraka inatumia Balozi za Tanzania nje ya nchi katika kutafuta fursa za masoko ya Mazao  na bidhaa pamoja na kuanzisha madawati ya biashara (Trade/Commercial attache) Kwenye balozi hizo.

Pia amesema mpango mkakati wa kuwaunganisha wakulima na wasindikaji ndani na nje ya nchi ni muhimu kutekeleza haraka iwezekanavyo ikiwa ni pamoja na kujenga uwezo zaidi katika kuongeza Uzalishaji wenye tija ili kukidhi nahitaji ya soko la ndani na nje ya nchi.  

Kadhalika Waziri Bashungwa ameongeza kuwa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) na Bodi ya Nafaka na Mazao Mchanganyiko (CPB) wanapaswa kukutana na Shirika la Chakula Duniani (WFP) kujadili uimarishaji wa masoko ya Mazao mbalimbali.

Pamoja na mambo mengine Waziri Bashungwa ameitaka Taasisi ya kuendeleza Kilimo Barani Afrika (AGRA) kushirikiana na wadau wengine wa sekta ya Kilimo ili kutafuta ufunguzi wa namna ya kuimarisha masoko ya Mazao ya wakulima nchini.

MWISHO
Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com