METDO Tanzania

METDO Tanzania

Monday, April 6, 2020

CRDB YATOA TANI 4 ZA MBEGU KUMUUNGA MKONO MAMA SALMA KIKWETE


Benki ya CRDB jana  imekabidhi tani 4 za mbegu ya Mahindi, Mtama na Mpunga zenye thamani ya shilingi milino 20 kwa Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mhe Godfrey Zambi ikiwa ni msaada uliombwa na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) Mheshimiwa Mama Salma Kikwete (Mb) kwa benki ya CRDB  kwa ajili ya waathirika wa mafuriko yaliyotokea kwa Mkoa wa Lindi.


Akizungumza mbele ya waandishi wa habari Mkurugenzi wa Masoko,Utafiti na huduma kwa wateja CRDB Bi Tully Mwambapa amesema mbegu hizi zimetolewa kutokana na maombi maalumu waliyopata kutoka kwa Mhe. Mama Salma Kikwete.

Aidha Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mhe Godfrey Zambi alitoa shukrani zake za dhati kwa CRDB pamoja na Mhe. Mama Salma Kikwete kwa namna ambavyo amekuwa mstari wa mbele kushiriki kwa karibu kuwasadia waathirika wa mafuriko tangia yalipoanza kutokea Mkoa wa Lindi. Mkuu wa Mkoa alitoa wito kwa viongozi wengine kuiga mfano wa Mhe Mama Salma Kikwete.

Tukio hilo lilifanyika jana katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Lindi ambapo viongozi mbalimbali ngazi ya Mkoa walishiriki pamoja viongozi kutoka Taasisi ya WAMA akiwamo Ndugu Ally Kikwete Katibu Mkuu wa Taasisi ya WAMA.
Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com