METDO Tanzania

METDO Tanzania

Friday, March 13, 2020

NAIBU WAZIRI KILIMO AKASIRISHWA NA UTEKELEZAJI WA MIRADI YA ERPP WILAYA YA KILOSA NA MVOMERO-MOROGORO

Naibu waziri Akikagua Skimu ya Kilangali- Shamba la Uzalishaji wa Mbegu Bora za zao la Mpunga Chini ya Wakala wa Mbegu ASA
Ghala la Kijiji cha Kigugu Wilayani Mvomero likiwa katika hatua za umaliziajia,Ghala linajengwa kupitia Mradi wa ERPP
Naibu Waziri wa Kilimo Omary Mgumba akizungumza na Viongozi wa Wilaya ya Kilosa pamoja na Wakandarasi katika Skimu ya Umwagiliaji Kijiji cha Mvumi.

NAIBU waziri wa Kilimo Omary Mgumba amefanya ziara katika Mradi wa kuongeza Tija zao la Mpunga ERPP Katika Wilaya ya Kilosa na Mvomero Mkoani Morogoro,huku akieleza kuchukizwa kutokana na kasi ndogo ya wakandarasi ya utekelezaji wa mradi huo Katika ujenzi wa skimu za umwagiliaji pamoja na Maghala.
Mradi wa ERPP wa unatekelezwa na wizara ya Kilimo ukiwa na lengo la kuongeza Tija katika  uzalishaji wa zao la Mpunga  kwa kutoa mbegu bora za zao hilo ukarabati na ujenzi wa Skimu na sambamba na Mgahala.
Akiwa katika Kijiji cha  Mvumi Wilayani Kilosa Mgumba amesema kuwa Hajaridhishwa na Ujenzi wa mifereji,pamoja na barabara katika skimu hiyo unaosimamiwa na Mkandarasi wa Kampuni ya White City International ya Jijini Dar es salaam kutokana na kasi ndogo ya ujenzi huku ikionekana kujengwa chini ya kiwango.
Aidha amesema kuwa ana mashaka ya kushindwa kumalizika kwa wakati wa mradi huo kwa wakati kutokana na kasi ambayo inaonyeshwa ana mkandarasi huyo ambapo anahitajika kumalizika April 21 mwaka huu.
Sanjari na hayo Naibu waziri Kilimo ametembelea Shamba la kuzalisha mbegu la Mpunga la Kilangali ambalo lipo chini ya Wakala wa Mbegu Nchini ASA na Wizara hiyo kupitia Mradi wa ERPP  wanajenga mifereji (SKIMU) ambayo kampuni ya Lukolo ndiyo iliyopewa kazi hiyo kwa gharama za Bilioni 4.5.
Aidha ameitaka kampuni hiyo kuongeza kasi ya ujenzi ili uweze kukamilika kwa wakati jambo ili shamba hilo liweze kuzalisha kwa wingi mbegu la Mpunga
Amesema kuwa matarajio ya Serikali ni kuona wananchi wake wananufaika na Mradi wa ERPP Lakini kampuni hizo zinarudisha nyuma jitihada hizo za serikali kutokana miradi hiyo kucheleweshwa
Akiwa katika Halmsahauri ya Wilaya ya Mvomero Mkoani Morogoro Mgumba alitembelea Skimu ya  umwagiliaji Kijiji cha Kigugu  ambapo kampuni ya GOPA na kukuta kazi haiendelee vizuri
Mhe Omary Mgumba akizungumza mara baada ya kukagua amesema kuwa mkandari huyo anafanya kazi taratibu jambo ambalo alimtaka wakutane nae ofisini kwake Jijini Dodoma ili kujua chanzo cha kufanya kazi taratibu
Awali akiwa katika Wilaya ya Kilosa Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Hassan Mkopi alisema kuwa Mkandarasi wa kampuni ya White City amejenga barabara hiyo chini ya kiwango kwa kutumia vifusi ambavyo sio sasa licha ya ushauri ambao alikuwa akiupata kutoka kwa wakazi wa eneo la Mvumi
Mkopi amesema kuwa Mkandari huyo amekuwa na ushirikiano mdogo na wananchi licha mradi huo kuwa wao ndio wanufaika wakuu.
Nao Baadhi  Maafisa Kilimo kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero wamesema kuwa miradi ya ERPP katika Wilaya hizo bado inasusua huku wakiomba serikali kuingilia katika suala hilo na wananchi waweze kuzalisha kwa tija kama lilovyokuwa lengo la serikali pamoja na mradi huo.
Mradi wa ERPP umetajwa kuleta mafanikio  makubwa kwa wakulima kwa kuongeza mavuno kutokana na elimu ambayo wamekuwa wakipatiwa .
Hata hivyo kukamilika kwa maghala pamoja na skimu za umwagiliaji kutaongeza tija zaiadi kwa wakulima kwani kutawawezesha kulima kibiashara zaidi tofauti na hapo awali.
Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com