METDO Tanzania

METDO Tanzania

Thursday, March 5, 2020

MKE WA RAIS MAMA JANETH MAGUFULI AKABIDHI VITI VYA MWENDO (WHEELCHAIRS) KWA WABUNGE KWA AJILI YA WATOTO WENYE ULEMAVU


Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akipokea shukurani za bila kushikana mikono na Mbunge wa Kilombero (kupitia tiketi ya CHADEMA) Mhe. Peter Ambrose Paciens Lijualikali baada ya kumkabidhi viti mwendo (Wheelchairs) 10 kwa ajili ya watoto wenye Ulemavu wakati wa hafla fupi iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam leo Alhamisi Machi 5, 2020. Wanaoshuhudia ni Naibu Spika wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Tulia Ackson na Mke wa Balozi wa Tanzania nchini Israel Mama Joan Masima.
Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akiwa ameketi na  Naibu Spika wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Tulia Ackson, Naibu Waziri  Ofisi ya Waziri Mkuu (watu wenye ulemavu) Mhe. Stella Alex Ikupa, Mke wa Balozi wa Tanzania nchini Israel Mama Joan Masima na mkuu wa Wilaya ya Ilala Mhe. Sofia Mjema katika picha ya pamoja na wabunge na wawakilishi wa wabunge baada ya kuwakabidhi viti mwendo (Wheelchairs) 210 kwa  ajili ya watoto wenye Ulemavu wakati wa hafla fupi iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam leo Alhamisi Machi 5, 2020.
Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akisalimiana na  Naibu Spika wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Tulia Ackson, baada ya kuwakabidhi wabunge viti mwendo (Wheelchairs) 210 kwa ajili ya watoto wenye Ulemavu wakati wa hafla fupi iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam leo Alhamisi Machi 5, 2020.
Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akisalimiana na  Mama Ulega, mke wa Mbunge wa Mkuranga na Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe, Abdallah Ulega baada ya kuwakabidhi wabunge viti mwendo (Wheelchairs) 210 kwa ajili ya watoto wenye Ulemavu wakati wa hafla fupi iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam leo Alhamisi Machi 5, 2020. (kushoto ni Naibu Spika wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Tulia Ackson na Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (watu wenye ulemavu) Mhe. Stella Alex Ikupa
Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com