METDO Tanzania

METDO Tanzania

Wednesday, March 4, 2020

MENEJA WA TANROAD MORO AREJESHWE WIZARANI-MAJALIWA

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua kazi ya ukarabati wa daraja la Kiyegeya  lililopo  eneo la Gairo ambalo limesombwa na maji   na kusababisha kukatika kwa mawasiliano kati ya Morogoro na Dodoma, Machi 4, 2020. Wa pili kulia ni Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi  Isack Kamwelwe. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) 
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua kazi ya ukarabati wa daraja la Kiyegeya lililopo eneo la Gairo  ambalo llimesombwa na maji  na kusababisha kukatika kwa mawasiliano  ya barabara ya barabara kati ya Morogoro na Dodoma, Machi 4, 2020. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 Eneo la daraja la Kiyegeya  ambalo lilisombwa na maji na kusababisha kukatika kwa mawasiliano ya barabara kati ya Morogoro na Dodoma , ukarabati wake unaendelea. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameagiza Meneja wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROAD), mkoa wa Morogoro, Mhandisi Godwin Andalwisye arejeshwe wizarani na nafasi yake ijazwe na mtu mwingine mara moja baada ya kuzembea kutimiza wajibu wake.
Uamuzi huo umekuja baada ya kiongozi huyo kushindwa kufanya ukaguzi wa usala wa madaraja yaliyoko kwenye mkoa wake na kubaini kama kuna daraja linamatatizo hali iliyosababisha daraja la Kiyegea lililopo eneo la Gairo ambalo linaunganisha mkoa wa Morogoro na Dodoma kuvunjika.
Waziri Mkuu ameyasema hayo leo(Jumatano, Machi 4, 2020) baada ya kutembelea eneo hilo na kukagua ukarabati ili kurejesha mawasiliano ya barabara. Waziri Mkuu ameshuhudia mrundikano wa magari na abiria hali ambayo haikumfurahisha.
“Hivi unajua udhahifu wako ni kwa sababu hukufanya ukaguzi kuona kama daraja limejaa mchanga au uchafu ambao umesababisha kipenyo cha kupitisha maji kuwa kidogo na maji yakalazimika kupanda juu hali ambayo ilisababisha daraja hili kusombwa na maji.”
Amesema wakati njia hiyo inarekebishwa itengenezwe njia nyingine ya muda ili kuweza kupitisha magari na kisha Serikali itachukua hatua baada ya kubaini nini kimesababisha.  
Ili kuharakisha kazi hiyo inakamilika kwa haraka, Waziri Mkuu ameagiza Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi, Mhandisi Isack Kamwelwe, Katibu Mkuu wa wizara hiyo pamoja na wahandisi wote wa TANROAD mkoa wa Morogoro na Dodoma leo wakutane kwenye eneo la tukio na wahakikishe kuanzia kesho (Alhamisi, Machi 5, 2020) njia hiyo iwe imefunguka.
Kadhalika, Waziri Mkuu amesema atawasiliana na Mkuu wa Majeshi, Generali Venance Mabeyo ili aweze kupata msaada wa wanajeshi ili waongeze nguvu katika kuhakikisha kwamba mawasialaino yanarejea kwa haraka.
Akiwapa pole madereva na watumiaji wengine wa barabara waliokwama katika eneo hilo, Waziri Mkuu amesema “Nimetumwa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli kuja kuwapa pole na kuwahakikisha kwamba Serikali inafanya kila linalowezekana ili kuifungua barabara hii.”
Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com