METDO Tanzania

METDO Tanzania

Monday, March 30, 2020

KATIBU MKUU KILIMO GERALD KUSAYA AIAGIZA TUME YA UMWAGILIAJI KUJIKITA NA MIRADI MICHACHE NA IKAMILIKE KWA WAKATI




Na Bashiri Salum, Wizara ya Kilimo-Morogoro

Tume ya Umwagiliaji nchini imetakiwa kujikita katika miradi michache itakayo kamilika na kuleta tija kwa wakulima  kuliko kuwa na miradi mingi isiyokamilika.

Katika kipindi cha miaka  mitano kuanzia mwaka 2015 mpaka 2020 mkoa  wa Morogoro imekuwepo  miradi saba  inayotekelezwa katika wilaya  Zaidi ya 11 ambapo mingi haijakamilika kutokana na changamoto mbalimbali.

Akiongea na wahandisi wa Tume hiyo  katika ofisi  ya kanda iliyoko Morogoro Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Bw. Gerald Kusaya ameishauri Tume hiyo kuwa na miradi michache ambayo itakamilika kwa ufanisi mkubwa.

Amesema Tume ya Umwagiliaji  kwa sasa ina deni kubwa kwa wakulima na wananchi  kwa ujumla  ambao wamepoteza Imani  na tume hiyo.

“Fanye kila litakalowapendeza mhakikishe mnarudisha Imani kwa wananchi na Raisi wa Jamhuri ya muunganoo wa Tanznania Mhe. Dkt John pombe magufuli” alisema Bw Kusaya

Akitolea mfano wa skimu za umwagiliaji za Kilangali, Msola Ujamaa  na Kigugu amesema matatizo ya skimu hizi  yametokana na usimamizi usioridhisha na kutochukuwa hatua kwa wakandarasi hivyo kusababisha wakulima kushindwa kufikia malengo yao.

Aidha Katibu Mkuu amewataka wahandisi hao kufanya kazi kwa  ushirikiano na kujiamini wakati wakitambua kuwa Tume inamchango mkubwa katika kubadilisha Maisha ya wakulima na taifa kwa ujumla.

Hata hivyo Bw. Kusaya ameitaka tume kuyatangaza mambo mazuri wanayoyafanya  kupitia vyombo vya Habari ili wadau waweze kuifahamu tumena kwa kuwa mambo mengi yanatokana na kutokuwa na taarifa sahihi.

Awali akitoa taarifa kwa Katibu Mkuu na viongozi wengine walioambatana nao Kaimu Mhandisi umwagiliaji mkoa wa Morogoro Njanji Mlwale amesema changamoto ya ukosefu wa fedha kulingana na mahitaji umechangia kwa kiasi kikubwa miradi mingi kuto kamilika.

Mhandisi Njanji amebainisha kwamba umekuwepo mgongano wa utekelezaji wa majukumu baina ya Tume na wataalamu walioko chini ya wakurugenzi watendaji wa Halmashauri mabalimbali ambao wanatekeleza shughuli za umwagiliaji kama ilivyo Tume.

Muingiliano huo wa majukumu umekuwa ukisababisha  miradi mingi ya Halmashauri kutokamilika na lwama kurudi kwa Tume ya Taifa ya umwagiliaji alisema Mhandisi.

Hata hivyo Mhandisi Njanji  amebainisha kwamba ukosefu wa maabara ya Tume ambayo ingesaidia katika vipimo mbalimbali imesababisha uchelewashaji wa miradi kwa kuwa  Pamoja na kugharimu fedha nyingi lakini sampuli zimekuwa zikichelewa.

MWISHO
Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com