Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ileje Haji
Mnasi akizungumza na walimu Wilayani Ileje mkoani
Songwe na wametakiwa kufuata taratibu za kazi
NA FREDY MGUNDA,ILEJE.
Walimu Wilayani Ileje mkoani
Songwe wametakiwa kufuata taratibu za kazi ili kuepusha kuwatwisha mizigo
Walimu wakuu na Wakuu wa Shule.
Wito huo ulitolewa hivi
karibuni na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ileje Ndg.Haji
Mnasi alipokuwa akifungua mafunzo ya siku moja kwa walimu wa Shule za Msingi za
Kata za Itumba na Isongole yaliyofanyika katika Shule ya Msingi Nyerere mjini
Itumba.
“Warahisisheni Walimu Wakuu
msiwape kazi ya kushitaki kwa usumbufu na kufikia kukataliwa na baadhi ya
walimu kwasababu ya usumbufu wenu”alisema kiongozi huyo.
Mnasi aliongeza kuwa,katika
ziara za kikazi alizozifanya kwenye baadhi ya Shule za Msingi na Sekondari
aliojionea hali isiyo ya kuridhisha ambayo inaonesha uwajibikaji wa kiwango cha
chini kinachoathiri hata matokea ya mitihani ya kitaifa.
Katika kikao hicho pia
alipongeza idara zote zinazohusika na masuala ya elimu kwa kuandaa mafunzo hayo
ambayo yanatarajiwa kufanyika kwenye kata zote za wilaya hiyo.
Kwa miaka ya hivi karibuni
wilaya ya Ileje imekuwa ikifanya vibaya kwenye mitihani ya Kumaliza Elimu ya
Msingi hali iliyopelekea viongozi hawa kukutana na walimu katika kukumbushana
mbinu za kujifunzia na kufundishia.
0 comments:
Post a Comment