METDO Tanzania

METDO Tanzania

Monday, February 24, 2020

WAZIRI WA MAENDELEO NA BIASHARA YA KIMATAIFA AKUTANA NA KATIBU MKUU WIZARA YA AFYA JOHN JINGU





Waziri wa maendeleo na biashara ya nje wa Finland Bw. Ville Skinnari na ujumbe wake alipokutana na Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Wizarani hapo, Jijini Dodoma leo tarehe 24/02/2020

Waziri wa Maendeleo na Biashara ya kimataifa wa Finland  Bw. Ville Skinnari amefanya mazungumzo na Katibu Mkuu, Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto(Idara Kuu ya Mendeleo ya Jamii), Dkt. John Jingu kuhusu maendeleo na usawa wa jinsia hapa nchini.

Akizungumzia masuala ya Jinsia, Katibu Mkuu Jingu amesema Serikali imechukua hatua madhubiti kuboresha usawa wa kijinsia na haki ya mtoto wa kike.

Amesema Serikali kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, imewekeza katika kuwawezesha wanawake kiuchumi na masuala ya uongozi.

Ameongeza kuwa Serikali imeweka mkakati kukabiliana na mimba katika umri mdogo na kupinga mila zilizopitwa na wakati ikiwemo ukeketaji.

Aidha, ameongeza kuwa sera ya Taifa ni kushirikisha wananchi katika jitihada za kukabiliana na vikwazo vilivyopo.

Dkt. Jingu amesema Serikali katika ngazi mbalimbali za uongozi imeunda kamati maalum za kulinda na kuhakikisha haki za mtoto zinalindwa.

Kwa upande wake, Waziri wa Maendeleo na Biashara ya Kimataifa kutoka Finland Bw.  Ville Skinnari amesema nchi yake inaunga mkono juhudi za Tanzania kupambana na changamoto zilizopo.
Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com