Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akizungumza kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt. John Pombe Joseph Magufuli leo tarehe 11 Februari 2020 wakati Mkutano wa 43 wa Magavana wa Mfuko wa Kimataifa wa Maendeleo ya Kilimo (IFAD) Jijini Roma nchini Italia. (Picha Zote Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo)
Sehemu ya washiriki wa Mkutano wa 43 wa Magavana wa Mfuko wa Kimataifa wa Maendeleo ya Kilimo (IFAD) unaofanyika Jijini Roma nchini Italia leo tarehe 11 Februari 2020, wakifuatilia mada mbalimbali zilizowasilishwa.
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akisalimiana na Rais wa Mali Mhe Ibrahim Boubacar Keita kabla ya kuanza Mkutano wa 43 wa Magavana wa Mfuko wa Kimataifa wa Maendeleo ya Kilimo (IFAD) unaofanyika Jijini Roma nchini Italia, leo tarehe 11 Februari 2020
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akizungumza wa baadhi ya washiriki wa Mkutano wa 43 wa Magavana wa Mfuko wa Kimataifa wa Maendeleo ya Kilimo (IFAD) Jijini Roma nchini Italia muda mfupi kabla ya kuanza kwa mkutano huo, Leo tarehe 11 Februari 2020.
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) leo tarehe 11 Februari 2020 akifatilia Mkutano wa 43 wa Magavana wa Mfuko wa Kimataifa wa Maendeleo ya Kilimo (IFAD) Jijini Roma nchini Italia.
Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo, Roma-Italy
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imekusudia kuendeleza ushirikiano maradufu baina yake na Mfuko wa Kimataifa wa Maendeleo ya Kilimo (IFAD) ili kuhakikisha kuwa inaendana na lengo la Jumuiya ya Kimataifa ya kufuta baa la njaa Duniani ifikapo mwaka 2030.
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akizungumza kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt. John Pombe Joseph Magufuli leo tarehe 11 Februari 2020 kwenye Mkutano wa 43 wa Magavana wa Mfuko wa Kimataifa wa Maendeleo ya Kilimo (IFAD) Jijini Roma nchini Italia amesema kuwa maendeleo ya Kilimo Tanzania yanachagizwa pia na ushirikiano na IFAD.
Amesema kuwa hivi karibuni, serikali kwa kushirikiana na IFAD zimeanzisha na kuunda mpango wa fursa za mkakati wa nchi (COSOP) 2016-2021 na walikubali kufanya kazi pamoja katika kubadilisha sekta ya kilimo nchini Tanzania katika sekta ndogo kama mimea, mifugo na uvuvi.
Pamoja na mambo mengine lakini Waziri Hasunga amesema kuwa IFAD imekuwa mshirika muhimu katika mipango ya ujenzi na fedha na miradi ambayo inalenga kupambana na umasikini katika maeneo ya vijijini na kuimarisha uwezekano wa kumaliza njaa kwa jumla. Ambapo imekuwa mbele katika kubadilisha shughuli za kilimo katika nchi nyingi zinazoendelea ikiwa ni pamoja na Tanzania.
Waziri Hasunga ameeleza shukrani za Tanzania kwa IFAD kwa miradi mbalimbali ambayo imekuwa ikitekelezwa katika nchi ya Tanzania huku akisisitiza kuwa serikali haitosubiri mpaka mwaka 2030 kumaliza njaa bali itafanya haraka iwezekanavyo kumaliza baa la njaa.
Amesema juhudi hizo ni kwa ajili ya kushughulikia changamoto za umasikini wa watu waishio vijijini kupitia mikakati ya maendeleo ya hali ya juu na mipango ya ukuaji wa uchumi.
Katika taarifa yake Mhe Hasunga amesema kuwa umuhimu na msingi wa kilimo nchini Tanzania hauwezi kutiliwa mkazo kwani uchumi wa Watanzania kwa asilimia kubwa unaimarika kulingana na shughuli za kilimo na hivyo kuchangia zaidi ya 28.7% ya jumla ya pato la Taifa; asilimia 30 ya mapato ya nje; Ajira 65.5% na nguvu kazi ikiwa inachangia kwa 66% ya vifaa vya viwanda ghafi katika nchi na pia 100% ya mahitaji ya chakula cha Taifa.
Kuhusu ukuaji wa uchumi nchini Tanzania, Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) amesema kuwa ukuaji ni asilimia 7 kwa upande wa Tanzania bara na asilimia 6.6 kwa upande wa Zanzibar japo sekta ya kilimo haijawahi kuongezeka kwa kiwango kinachohitajika kutokana na changamoto kadhaa ambazo zinajumuisha tija, mabadiliko ya hali ya hewa, teknolojia duni, matumizi duni ya soko na kilimo cha mazoea.
Kwa upande wake Balozi wa Tanzania nchini Italia Mhe George Kahema Madafa ameeleza namna ambavyo IFAD na Tanzania imeendelea kuimarisha dhamira yake ya Ushirikiano.
Amesema kuwa mkutano huo umekuwa muhimu kwa Tanzania kueleza hatua nzuri iliyonayo ya kimaendeleo na namna ambavyo imejipanga katika kuimarisha sekta ya maendeleo endelevu.
MWISHO
0 comments:
Post a Comment