Mbunge wa kuteuliwa na Mhe Rais lakini pia ni Mke wa Rais Mstaafu Mhe. Mama Salma Kikwete amekabidhi Mabati 760 kwa ajili ya wahanga wa Mafuriko bati 500, Ujenzi wa Ofisi ya Chama Halmashauri ya Mtama Bati 200 na Ujenzi wa Shule ya Sekondari Kata ya Mnara Bati 60.
Akizungumza katika kukabidhi mabati hayo Mama Salma Kikwete alisema “nimetoa bati hizi kwa kuwa mpaka sasa Chama hakina Ofisi na wenzetu wahanga wamepewa maeneo lakini bado wanaitaji msaada mkubwa katika kuhakikisha wanapata huduma pamoja na sehemu ya kuishi” Alikaririwa Salma Kikwete
Mama Salma Kikwete aliongeza kwa kusema “mimi nipo tayari kusaidia wahanga kwa chochote kama nilivyojitoa kuwapa mabati haya lakini nawaomba sana Watanzania kuendelea kuwasaidia wahanga wetu wa Mchinga, Kilwa na maeneo mengine ambayo bado wananchi wetu hawajapa sehemu muhimu ya kuishi" Alisema
Hata hivyo nae Katibu wa Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Lindi Vijijini Rukia Hassan amempongeza Mh Mama Salma Kikwete kwa kutoa bata 200 kwa ajili ya Ujenzi wa Ofisi katika Halmashauri.
0 comments:
Post a Comment