METDO Tanzania

METDO Tanzania

Wednesday, January 22, 2020

TUMIENI FURSA ZA UJIO WA UMEME KUBADILISHA MAISHA, MBUNGE WA CHALINZE RIDHIWANI KIKWETE

 MBUNGE wa Chalinze Mhe. Ridhiwani Kikwete, akihutubia kwenye mkutano huo Januari 21, 2020
 Naibu Waziri wa Nishati, Mhe. Subira Mgalu, akihutubia wananchi wa kijiji cha Talawanda Januari 21, 2020 wakati w aziara yake ya kukagua maendeleo ya upelekaji wa mradi wa umeme kwenye vijiji vya Talawanda na Kibindu jimbo la Chalizne Mkoani Pwani.
 Mhe. Kikwete akijadiliana jambo na wananchi wa jimbo lake huko kijiji cha Talawanda.
 Naibu Waziri wa Nishati, Mhe. Subira Mgalu akimsikiliza Mbunge wa jimbo la Chalinze Mhe. Ridhiwani Kikwete wakati wa ziara hiyo.
 MBUNGE wa Chalinze Mhe. Ridhiwani Kikwete, akihutubia kwenye mkutano huo Januari 21, 2020
 Baadhi ya wanakijiji wakisikiliza 
 Baadhi ya wanakijiji wakisikiliza 

MBUNGE wa Chalinze Mhe. Ridhiwani Kikwete amewataka wakazi wa kijiji cha Talawanda kutumia fursa za ujio wa nishati ya umeme kubadilisha maisha yao.

Mheshimiwa Kikwete ameyasema hayo wakati akihutubia wananchi kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya zahanati ya kijiji hicho ambapo Naibu Waziri wa Nishati Mhe. Subira Mgalu alifika kukagua maendeleo ya upelekaji wa mradi wa umeme kwenye kijiji hicho chini ya mpango wa REA awamu ya tatu mzunguko wa kwanza kwa wigo wa nyongeza (ADDENDUM).

“Ndugu zangu tutumie vizuri rasilimali hii inayokuja, ukienda pale Chalinze miaka 25 iliyopita haikuwa Chalinze unayoiona leo, lakini leo ukienda pale mambo yamebadilika, watu wanaweza kufanya kazi mchana wakatijua linawaka na usiku jua linapopotea kwa sababu ya nishati ya umeme.

” Alisema Mhe. Kikwete na kuongeza, Lakini pia hata vyakula mtunavyokula sasa, zamani tulikata miti kwa kiwango cha juu kwa matumizi ya nyumbani, matokeo yake tunageuza eneo letu jangwa sasa hivi inaelekea tatizo hilo kuisha kwa sababu umeme umekuja.

Pia amesema Serikali inaendelea na ujenzi wa mradi mkubwa wa umeme wa Julius Nyerere kule Rufiji, mradi ukiisha kituo kikubwa cha kupoza umeme kitajengwa Chalinze na hivyo wanakijiji wa Talawanda na wana Chalizne wote wanapaswa kutumia fursa hizo ipasavyo.

Mbunge huyo wa Chalinze amelipongeza Shirika la umeme nchini TANESCO na wakala wa umeme vijijini REA kwa kasi ya upelekaji umeme kwenye maeneo ya vijiji vya jimbo la Chalinze ambapo umeme unaenda kuleta mabadiliko makubwa ya maisha ya wananchi.
Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com