Na
Mathias Canal, Dodoma
Mbunge wa Viti Maalum Mhe. Khadija Shaaban Taya (Keisha) amewaomba watu wenye ulemavu kuchangamkia fursa za kiuchumi zilizopo na kutoa ufafanuzi kuhusu Suala la Bandari ya Dar es salaam kwani linakwenda kugusa maisha ya watanzania.
TAYA amewataka
watu wenye ulemavu kuchangamkia fursa ambazo Serikali inazitengeneza ikiwemo
fursa za ajira zinazotangazwa.
Amesema kuwa Ofisi ya Waziri Mkuu
imekuwa ikitenga fedha kwa ajili ya kuwainua wananchi kiuchumi, kukuza ujuzi
lakini mwamko wa watu wenye ulemavu kushiriki katika fursa hizo umekuwa mdogo
sana.
Ameyasema hayo leo Jijini Dodoma wakati wa
hafla ya chakula cha mchana na watu wenye ulemavu iliyoandaliwa yeye mwenyewe iliyofanyika katika ukumbi wa
mkuu wa mkoa wa Dodoma.
Kuhusu sakata la bandari kuendeshwa na DP
WORLD, Mbunge Taya amewataka watu wenye ulemavu nchini kuacha kutishwa na
kuogopa maneno yanayoongelewa mtaani juu ya makubaliano baina ya Serikali ya
Tanzania na Serikali ya Dubai kuhusu ushirikiano wa kiuchumi na kijamii kwa
ajili ya uendelezaji na uboreshaji wa utendaji kazi wa bandari nchini namatokeo
yake wachangamkie fursa hiyo ili kuweza kujikwamua kiuchumi.
Mgeni rasmi katika hafla hiyo ya chakula cha
Mchana na watu wenye ulemavu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Ajira, Kazi,
Vijana na watu wenye Ulemavu) Mhe Prof. Joyce Ndalichako amesema Serikali
inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt. Samia Suluhu
Hassan inaendelea kuweka fursa mbalimbali kwaajili ya watu wenye ulemavu
ikiwemo kuwawezesha kufanya ujuzi na bunifu kwa kuwajengea Vyuo vya Ufundi.
Mhe Ndalichako
amesema kuwa Serikali imetenga jumla tsh. Bilioni tatu kwaajili ya
ujenzi wa vyuo vya watu wenye ulemavu hiyo ni kwa ajili ya kuendeleza vyuo
hivyo.
Prof. Ndalichako amesema mpaka sasa wanajenga
vyuo vipya vitatu vya watu wenye ulemavu kwa mikoa mitatu ikiwemo Kigoma,
Songwe na Ruvuma na kuwataka kuchangamkia fursa zinazotolewa kwenye mikopo yao.
MWISHO
0 comments:
Post a Comment