Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akipata maelezo kuhusiana na Mradi wa Nyumba za Shirika la Nyumba za Taifa (NHC) uliopo eneo la Ilembo Manispaa ya Mpanda mkoa wa Katavi kutoka kwa Meneja Mawasiliano wa Shirika hilo Muungano Saguya jana wakati akikagua utekelezaji wa miradi ya NHC mkoani Katavi. Wa kwanza kulia ni Mkuu wa wilaya ya Mpanda Lilian Matinga na kushoto ni Kaimu Meneja wa NHC mkoa wa Katavi na Rukwa Msumbuko Majaliwa.
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akioneshwa eneo inapojengwa ofisi ya Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) katika halmashauri ya wilaya ya Mlele mkoa wa Katavi na Meneja wa TFS Mlele Godfrey Mlele (Kulia) wakati wa ziara yake ya kukagua miradi inayotekelezwa na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) katika mkoa wa Katavi jana. Wa pili kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Mlele Recho Kasanda na wa pili kulia ni Meneja Mawasiliano wa NHC Muungano Saguya (PICHA ZOTE NA WIZARA YA ARDHI).
Na Munir
Shemweta, WANMM KATAVI
Naibu
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula amelipongeza
Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) mkoa wa Katavi kwa kuwa moja ya mkoa wenye
miradi mingi ya Shirika hilo.
Dkt
Mabula alitoa pongezi hizo jana wakati akikagua miradi ya NHC kwenye mkoa wa
Katavi akiwa katika ziara yake ya kukagua utendaji kazi wa sekta ya ardhi
pamoja na ujenzi wa miradi inayotekelezwa na Shirika la Nyumba la Taifa.
Miradi
aliyoikagua Naibu Waziri Mabula katika mkoa wa Katavi ni ujenzi wa nyumba za
watumishi katika Halmashauri ya wilaya ya Mlele, Ofisi na Nyumba ya Wakala wa
Huduma za Misitu Tanzania (TFS) pamoja na ukumbi wa halmashauri ya Manispaa ya
Mpanda. Pia alikagua mradi wa nyumba sabini za Ilembo ambapo Nyumba kumi kati
ya hizo ziliuzwa na nyumba sitini zimepangishwa.
Alisema,
mkoa wa Katavi unaweza kuwa mkoa wa kwanza ama wa pili kwa kuwa na miradi mingi
ya Shirika la Nyumba la Taifa na hali hiyo siyo tu inaonesha jinsi Shirika
lilivyo makini kwenye uwekezaji miradi mbalimbali kama vile ujenzi wa nyumba za
kuuza, kupangisha na majengo ya biashara bali inalifanya kuimarika kimkoa.
Akigeukia
mradi wa Jengo la Biashara la Paradise lililopo Manispaa ya Mpanda, Dkt Mabula
alilisifu jengo hilo kwa kuwa na mazingira mazuri ya kibiashara na kushauri
taasisi za serikali katika mkoa wa Katavi kutumia fursa ya kupanga na kuwekeza
kwenye jengo hilo kwa kuwa gharama zake ni nafuu ukilinganisha wapangishaji
wengine.
Aidha,
amelitaka Shirika la NHC mkoa wa Katavi kuhakikisha inalifanyia matangazo jengo
hilo la biashara la Paradise kwa lengo la kuvutia wateja kupanga hasa
ikizingatiwa kutolitangaza kunaweza kusababisha kukosa wateja.
Kauli
hiyo ya kutaka kufanyika matangazo kwenye jengo hilo inafuatia Naibu Waziri
Mabula kuelezwa na Kaimu Meneja wa Shirika la NHC mkoa wa Katavi na Rukwa
Masumbuko Majaliwa kuwa mpaka sasa jengo hilo la kibiashara limepangisha
asilimia thelathini tu ya wateja.
‘’Mrudi
kwenye kutangaza miradi yenu kupitia kipindi cha Maisha ni Nyumba na
ikiwezekana kazi hiyo ifanyike mkoa kwa mkoa na mhakikishe miradi yenu
mnaifanya kwa kasi, viwango na wakati ili kujenga trust kwa wateja’’ Alisema
Dkt Mabula.
Kwa
upande wake Meneja Mawasiliano wa NHC Muungano Saguya alisema, kwa sasa Shirika
lake linafanya vizuri katika masuala ya ujenzi jambo lililosababisha kuaminwa
na serikali ambapo katika mji wa serikali eneo la Mtumba Dodoma liliweza
kujenga majengo ya Wizara nne na sasa Shirika linaendelea na utekelezaji wa
miradi mingine kama vile ujenzi wa nyumba na ofisi za Wakala wa Huduma za
Misitu Tanzania (TFS) nchi nzima.
Awali
Kaimu Meneja wa Shirika la Nyumba mkoa wa Katavi na Rukwa Masumbuko Majaliwa
alimueleza Naibu Waziri kuwa kwa sasa NHC mkoa wa Katavi inatekeleza miradi
mbalimbali katika mikoa ya Katavi na Rukwa.
Alisema
katika mkoa wa Katavi Shirika la Nyumba linatekeleza miradi ya nyumba za
watumishi Mlele, ukumbi wa manispaa ya Mpanda pamoja na ujenzi wa nyumba za
walimu Kibaoni wakati upande wa mkoa wa Rukwa miradi inayotekelezwa ni ile ya
mradi wa nyumba za makazi jangwani Sumbawanga pamoja na duka la dawa katika
hopspitali ya rufaa mkoa wa Rukwa.
0 comments:
Post a Comment