Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani (katikati) akikata utepe kuashiria kuwasha umeme katika kijiji cha Nyantimba wilayani Chato mkoani Geita.
Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani (kushoto) akipokea zawadi kutoka katika kikundi cha kimama wa kijiji cha Nyantimba wilayani Chato mkoani Geita, ikiwa ni zawadi yao kwa waziri huyo baada ya kufika kijijini hapo.
Baadhi ya watoto wakazi wa Kijiji cha Nyantimba wakimsikiliza Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani( hayupo pichani) alipofika katika kijiji hicho kilichopo wilayani Chato mkoani Geita kuwasha umeme.
Waziri wa Nishati, Dkt. Medadrd
Kalemani amesema mvua nyingi zinazoendelea kunyesha katika maeneo mbalimbali
nchini kwa sasa zimesababisha baadhi ya maeneo kukatika umeme mara kwa mara ama
kukosa huduma huyo.
Dkt. Kalemani alitoa kauli hiyo,
katika Wilaya ya Chato mkoani Geita, wakati ziara yake ya kukagua maendeleo ya
usambazaji umeme vijijini, ambapo pamoja na mambo mengine aliwasha umeme katika
Vijiji vya Nyantimba na Kanyindo katika wilaya hiyo, Januari 22,2020.
Alisema kuwa mvua zinazonyesha
zimeambatana na upepo mkali ambao husababisha baadhi ya miundombinu ya umeme
kuangua na nyaya kuungua moto kutokana na kugusana, hivyo kusababisha hitilafu
na maeneo mengi kukosa huduma ya umeme, akitolea mfano maeneo ya Jiji la Dar Es
Salaam na Mkoa wa Morogoro.
Dkt. Kalemani, alisema umeme
unaozalishwa nchi kwa sasa ni mwingi na wa kutosha kukidhi mahitaji ya nchi na
ziada, hivyo tatizo la kukatika kwa umeme ama kukosekana kwa huduma hiyo hakumaniishi
kwamba umeme unaozalishwa hautoshi la hasha.
Sambasamba na hilo alisema kuwa,
kutokana na hali hiyo wakati mwingine mafundi wanalazimika kuzima umeme katika
baadhi ya maeneo ili kufanya ukarabati wa miundombinu iliyoharibika.
“Hizi mvua kubwa zinazoendelea
kunyesha nchini zinasababisha nguzo kuanguka,nyaya kugusana na nyaya zikigusana
zinaungua na kusababisha umeme kukatika katika baadhi ya maeneo,siyo kwamba
umeme hautoshi hapana, umeme upo mwingi na wakutosha mahitaji yetu”, alisema
Dkt. Kalemani.
Aliwataka wananchi kuwa wavumilivu na
kuvuta subira pamoja na kutoa ushirikiano kwa sekta husika wakati Serikali inaendelea
kukarabati na kuimarisha miundombinu ya umeme nchi nzima ili kuweza kukabiliana
na changamoto zinazojitokeza.
Akizungumzia suala la usambazaji wa
umeme vijijini, Dkt. Kalemani alitoa mwezi mmoja kwa Shirika la Umeme Tanzania
(TANESCO)kuwaunganishia umeme wananchi wote wa Kata ya Nyalutembo wilayani
Chato mkoani Geita waliopo katika mpango wa kuunganishiwa umeme na ambao
wamekwisha lipia.
Kata hiyo ya Nyalutembo yenye vijiji vinne ambavyo
baadhi ya wakazi wake wamelipia huduma ya umeme lakini mpaka sasa bado
hawajaunganishwa kutokana na sababu mbalimbali.
Aidha aliwataka wananchi hao, kulipia
shilingi 27,000 tu, ili kuunganishiwa umeme, pia wasikubali kutozwa gharama za
nguzo, LUKU wala nyaya kwa kuwa gharama hizo tayari zimelipwa na serikali.
Kata hiyo inaunganishiwa umeme na
TANESCO, ikiwa ni mpango wa wake wa kusambaza umeme vijijini kwa gharama nafuu
kama ilivyo kwa Wakala wa Nishati Vijijini (REA).
Wakazi wa maeneo hayo walitakiwa
kuongeza kasi kulipia huduma hiyo na kutandaza nyaya katika nyumba zao, hata
kama miundombinu imepita mbali na makazi yao na kwamba wasisubiri nguzo
ziwafikie kwa kuwa lengo la serikali ni kuwafikishia umeme wananchi wote katika
nyumba zao na kwa bei nafuu.
“Wananchi nawasisitiza kulipia
gharama, na kutandaza nyaya katika nyumba zenu, msisubiri nguzo hii siyo kazi
yenu, ni kazi ya serikali kuwaleta nguzo katika maeneo yenu, sasa nyie changamkieni
fursa na muwe tayari ili siku mkifikiwa iwe rahisi na haraka kuunganishiwa”,
alisisitiza Dkt. Kalemani.
Aliwaeleza wanakijiji hao kuwa,
watumie umeme huo kwa manufaa na kujiletea maendeleo kwa kuanzisha viwanda
vidogo na biashara mbalimbali zenye kuinua vipato vyao tofauti na ilivyokuwa
kabla ya kupata umeme.
0 comments:
Post a Comment