Mkurugenzi wa Shirika linalojishughulisha na Ufadhili wa Wanafunzi wa kike
CAMFED, Bi.Lydia Wilbard akifafanua jambo kwa Waandishi wa Habari(hawapo
pichani), kuhusu wanafunzi 9,877 wa kike watakaofadhiliwa masomo yao ya
Sekondari mwaka huu 2020, kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi CAMFED, Bi.Jeane
Ndyetabura.
Mkurugenzi wa Shirika linalojishughulisha na Ufadhili wa Wanafunzi wa kike
CAMFED, Bi.Lydia Wilbard akifafanua jambo kwa Waandishi wa Habari(hawapo
pichani), kuhusu wanafunzi 9,877 wa kike watakaofadhiliwa masomo yao ya
Sekondari mwaka huu 2020.
Mwenyekiti wa Bodi CAMFED, Bi.Jeane Ndyetabura, akifafanua jambo kwa
Waandishi wa Habari (hawapo pichani), kuhusu wanafunzi 9,877 wa kike
watakaofadhiliwa masomo yao ya Sekondari mwaka huu 2020, kulia ni Mkurugenzi
Mkuu CAMFED, Bi. Lydia Wilbard.
Mkurugenzi wa Shirika linalojishughulisha na Ufadhili wa Wanafunzi wa kike
CAMFED, Bi.Lydia Wilbard na wafanyakazi wengine kutoka shirika hilo akiwa
kwenye picha ya pamoja na Wawakilishi wa wanafunzi wa kike wanaofadhiliwa na
Shirika hilo mara baada ya mkutano na waandishi wa habari leo Januari 27, 2020
Jijini Dar es Salaam.
Katika kuadhimisha siku ya Elimu Duniani inayoazimishwa kila mwaka tarehe 24
Januari, Shirika lisilo la kiserikali linalojishughulisha na kuwafadhili wanafunzi wa
kike wanaokutana na vikwazo mbalimbali ikiwemo vifaa vya shule, sare za shule na
unyanyasaji wa kijinsia CAMFED, limesifu jitihada za Serikali ya Awamu ya Tano ya
kutoa Elimu bure kuanzia shule ya Msingi hadi Sekondari.
Akizungumza katika Mkutano na Waandishi wa Habari Jijini Dar Es Salaam,
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika hilo, Bi.Lydia Wilbard alisema kuwa wamekuwa
wakifanya kazi kubwa kuwainua watoto wa kike ambao wanapitia katika mazingira
magumu ili wapate elimu katika kiwangi kinachostahili,na kwamba kwa sasa kazi
yao imekuwa rahisi kutokana na serikali kutoa elimu bure.
“Katika kuadhimisha siku ya elimu duniani CAMFED tumeendelea kupanua wigo
katika maeneo mengi zaidi nchini na kuweza kuzifikia shule za sekondari 471 katika
halmashauri 32, na programu hii imewezesha wanafunzi 50,000 wa kike kufanikisha
masomo yao ya Sekondari”, Alisema Bi. Wilbard.
Aidha katika kutekeleza majuku yao ya kuwasiadia wanafunzi wa kike ili kufikia
malengo yao, Bi. Wilbard alisema kuwa CAMFED kwa mwaka huu inalenga
kuwasaidia wanafunzi 9,877 kutimiza malengo yao ya kusoma sekondari na tayari
kiasi cha Sh. Bilioni mbili zimeshatolewa kuwasadia wanafunzi hao wa kike
kulingana na mahitaji ya kila mwanafunzi.
Alisema katika miaka ya nyuma CAMFED ilikuwa na jukumu kubwa la kugharamia
mahitaji ya mwanafunzi ikiwemo michango ya shule, Ada na mahitaji mengine
ambayo wanufaika wa program hiyo walihitajika kupata lakini baada ya Serikali ya
Awamu ya Tano kuingia madarakani na kutoa elimu bure wameweza kusaidia
wanafunzi wengi zaidi baada ya jukumu la ada kuchukuliwa na Serikali.
“ Kuondolewa kwa ada ya shule mwaka 2015 imewezesha wanafunzi wengi kupata
urahisi wa kusoma shule, lakini kwa wanafunzi wa kike walioko kwenye mazingira
magumu wanapata ugumu wa kwenda shule kwa sababu ya kukosa vifaa vya shule,
sare na mahitaji mengine ambayo mtoto wa kike anapaswa kuyapata, kwa hiyo
elimu bure imepunguza mzigo wa familia duni”, Alisema Bi.Wilbard.
Aliongeza kuwa CAMFED ambayo hasa inawanafunzi wa kike ambao waliwahi
kunufaika na mradi huo wamekuwa wakifanya kazi ya kuelimisha jamii na kuwapa
matumaini wanafunzi walioacha shule hatimaye kurejea mashuleni ambapo zaidi
ya wanafunzi 5,500 wa kike waliweza kurejea shuleni na kuendelea na masomo.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa bodi wa CAMFED, Bi. Jeane Ndyetabura alisema
kuwa Shirika hilo lililkuwa na mfumo maalumu wa kuwatambua wanafunzi walioko
kwenye mazingira magumu na kwenye hilo iligundulika kuwa watoto wa kike
wanapitia katika hali ngumu Zaidi.
“Tulikuwa na mfumo maalumu ambao ulitutambulisha kuwa watoto wa kike ambao
wako kwenye mazingira hatarishi ikiwemo umasikini, uhitaji mkubwa wa kiushauri,
kukosa wazazi wote na kuwekwa kwenye malezi mengine ambayo hayaendani na
ndoto zao za kupata elimu na sasa CAMFED inafanya kazi kubwa kuwainua popote
pale walipo ilimradi tu imekutana nao”, Alisema Bi.Ndyetabura.
0 comments:
Post a Comment