Makocha
20 wa Tanzania wanaofanya kozi ya Leseni A kutoka Shirikisho la Mpira wa
Miguu Afrika (CAF), wamemaliza kozi hiyo hatua ya kwanza na kusema,
“Tumenolewa na sasa tumeiva vya kutosha,” amesema mmoja wa wanafunzi
hao, Wilfred Kidao leo saa Julai 30, 2016 wakati Rais wa Shirikisho la
Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi.
Kidao
amesema japo kozi hiyo ilikuwa hatua ya kwanza ‘Module 1’ kwa sasa
wameiva kiasi kwamba watakapomaliza Novemba, mwaka huu wana uhakika wa
kupeleka vyeti vyao sehemu yoyote duniani kuomba kazi na kushinda kwa
kuwa wameiva vilivyo. Wakufunzi wa kozi hiyo walitokea CAF, Sunday
Kayuni na Salum Madadi ambaye ni Mkurugenzi wa Ufundi wa TFF.
Baada ya
kusikiliza kauli hiyo ya Kidao, Rais wa TFF Jamal Malinzi moja kwa moja
akawasisitiza makocha hao kufanya kazi kwa juhudi na kuwaeleza kuwa
hatua waliyofikia ni kubwa kwa kuwa baadhi ya makocha kutoka nje hawana
vyeti na kukosa sifa ya kufundisha timu kubwa ikiwamo timu za mataifa
ngazi mbalimbali.
Rais
Malinzi alitaka makocha hao kuangazia mpira wa miguu kwa wavulana wengi
wakiwa wanatokea katika mashindano yanayodhaminiwa na Kampuni ya simu ya
Airtel pamoja na soko la wasichana ambalo kwa sasa linashika chati kila
kona ya dunia.
Naye,
Makamu wa Rais wa TFF, Wallace Karia alimpongeza Rais Malinzi kwa namna
anavyoratibu na kuzikubali kozi mbalimbali za waamuzi na makocha. “Kwa
muda mrefu au tuseme kwa miaka mingi hakujafanyika kozi nyingi kama
kipindi cha uongozi wako ukisaidiana na mimi pamoja na kamati nzima ya
utendaji pamoja na sekretarieti.”
0 comments:
Post a Comment