METDO Tanzania

METDO Tanzania

Friday, December 6, 2019

WAZIRI MKUCHIKA AWATOLEA UVIVU WATUMISHI ”WANAOKALIA” BARUA ZA WENZAO


Waziri wa Nchi ofisi ya Rais Menejimenti, Utumishi wa Umma na Utawala bora Kapt Mstaafu Mhe.George Mkuchika akizungumza na waandishi wa habari  Jijini Dodoma Disemba 6,2019 wakati kuhusu maandhimisho ya siku ya maadili na haki za binadamu yatakayofanyika Disemba 11,2019 Jijini hapa
 
Mwenyekiti wa tume ya utumishi na utawala bora Jaji Harold Nsekela,akizungumza na waandishi wa habari  Jijini Dodoma Disemba 6,2019 wakati kuhusu maandhimisho ya siku ya maadili na haki za binadamu yatakayofanyika Disemba 11,2019 Jijini hapa
 
Sehemu ya viongozi wakifatilia hotuba ya Waziri wa Nchi ofisi ya Rais Menejimenti, Utumishi wa Umma na Utawala bora Kapt. Mstaafu George Mkuchika ,alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari  Jijini Dodoma Disemba 6,2019  kuhusu maandhimisho ya siku ya maadili na haki za binadamu yatakayofanyika Disemba 11,2019 Jijini hapa
Mwenyekiti Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora Bw.Mathew Mwaimu, akizungumza na waandishi wa habari  Jijini Dodoma Disemba 6,2019 kuhusu maandhimisho ya siku ya maadili na haki za binadamu yatakayofanyika Disemba 11,2019 Jijini hapa (kulia) ni Waziri wa Nchi ofisi ya Rais Menejimenti, Utumishi wa Umma na Utawala bora kapt.Mstaafu George Mkuchika
Naibu katibu mkuu Wizara ya Katiba na Sheria Amon Mpanju, akitoa ufafanuzi kwa  waandishi wa habari  Jijini Dodoma kuhusu maandhimisho ya siku ya maadili na haki za binadamu yatakayofanyika Disemba 11,2019 Jijini hapa (kulia) ni Waziri wa Nchi ofisi ya Rais Menejimenti, Utumishi wa Umma na Utawala bora Kapt.Mstaafu George Mkuchika
Mkurugenzi wa Idara ya Ukuzaji maadili katika Utumishi wa Umma Ofisi ya Rais -Utumishi Fabian Pokela,akizungumza na waandishi wa habari  Jijini Dodoma kuhusu maandhimisho ya siku ya maadili na haki za binadamu yatakayofanyika Disemba 11,2019 Jijini hapa
 
Sehemu ya watumishi wakifatilia Hotuba ya Waziri wa Nchi ofisi ya Rais Menejimenti, Utumishi wa Umma na Utawala bora Kapt.(MST) Mhe. George Mkuchika,wakati akitoa taarifa  kuelekea kilele cha Maadhimisho ya siku ya Maadili na Haki za Binadamu.
 Mwaandishi wa habari wa Gazeti la Mwananchi Habel Chidawali,akiuliza swali kwa  Waziri wa Nchi ofisi ya Rais Menejimenti, Utumishi wa Umma na Utawala bora Kapt.(MST) Mhe. George Mkuchika,wakati alipokuwa anatoa taarifa  kuelekea kilele cha Maadhimisho ya siku ya Maadili na Haki za Binadamu.
Sehemu ya waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali wakifatilia hotuba ya Waziri wa Nchi ofisi ya Rais Menejimenti, Utumishi wa Umma na Utawala bora Kapt.(MST) Mhe. George Mkuchika, alipokuwa akitoa taarifa  kuelekea kilele cha Maadhimisho ya siku ya Maadili na Haki za Binadamu.
Mwaandishi wa habari wa Gazeti la Tanzania Daima Danson Kaijage ,akiuliza swali kwa  Waziri wa Nchi ofisi ya Rais Menejimenti, Utumishi wa Umma na Utawala bora Kapt.(MST) Mhe. George Mkuchika,wakati alipokuwa anatoa taarifa  kuelekea kilele cha Maadhimisho ya siku ya Maadili na Haki za Binadamu.PICHA NA ALEX SONNA

…………….
Na.Alex Sonna,Dodoma
Waziri wa Nchi ofisi ya Rais Menejimenti, Utumishi wa Umma na Utawala bora Kepteni Mstaafu George Mkuchika amewakemea viongozi wa umma wanaokaa na barua za uhamisho wa watumishi bila kuwafikishi wahusika. 


Waziri Mkuchika ameyasema hayo leo jijini Dodoma wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na maandhimisho ya siku ya maadili na haki za binadamu yatakayofanyika Disemba 11,2019 Jijini hapa.


Amesema kuwa  kuna  baadhi ya viongozi wanachukua nafasi ya Katibu Mkuu Utumishi kwa kukaa na barua za wafanyakazi wao kinyume cha sheria za utumishi wa umma. 


” Ndani ya Serikali wapo viongozi wamekuwa na tabia ya kukaa na barua za uhamisho wa watumishi, unakuta mtu kaandika barua ya kuomba kuhamishwa lakini barua hiyo inapojibiwa viongozi wao wakiipokea hawaikabidhi kwa mhusika, wanakaa nayo,” amesisitiza Mhe. Mkuchika  

“Huu si utumishi bora kwani kiongozi huyo anaifanya Wizara kuonekana imechela kujibu barua hiyo, na Wizara inajua kuwa tayari mtumishi huyo kahamishwa, niwaambie kuwa kama mtumishi huyo bado unamuhitaji toa hoja za msingi ili asiondoke lakini si kukaa na barua yake,”.

Amesema ili kukabiliana na changamoto hiyo wanapanga kufanya semina kwa viongozi na watumishi wa umma Kuhusu utawala bora na misingi ya maadili.

Awali Mwenyekiti wa tume ya utumishi na utawala bora Jaji Harold Nsekela, amesema kuwa hapa nchini haki za binadamu zinafuatwa ipasavyo, kutokana na kwamba masuala ya uchumi yanaongezeka, elimu inatolewa bure na vingine vingi ambavyo vipo ndani ya maadili na hakiza binadamu.

Jaji Nsekela amesema kuwa  matarajio ya serikali ni kuhakikisha maadili yanaongezeka, kwa kusimamia sera na taraibu mbalimbali ambazo zinatakiwa kufanywa.

Maadhimisho hayo Kitaifa yatafanyika Desemba 11 katika ukumbi wa Pius Msekwa jijini Dodoma na yameratibiwa na na Taasisi zinazoshughulika na masuala ya haki za binadamu na utawala bora, kupambana na rushwa, uwajibikaji, usimamizi wa sheria ba maadili.
Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com