METDO Tanzania

METDO Tanzania

Saturday, December 7, 2019

RAIS DKT MAGUFULI AWEKA JIWE LA MSINGI LA UJENZI WA DARAJA LA KIGONGO-BUSISI (Km 3.2) JIJINI MWANZA LEO

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli
akiwa na viongozi mbalimbali akikata utepe kuanzisha rasmi kwa Ujenzi
wa Daraja la Kigongo-Busisi  lenye urefu wa Kilomita 3.2 kwenye
sherehe iliyofanyika Kigongo jijini Mwanza leo Desemba 7, 2019

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli
akisaidiwa na Spika wa Jamhuri ya Muungano Mhe Job Ndugai akifunua
kitambaa kuashiria uwekaji rasmi wa Jiwe la Msingi la Ujenzi wa Daraja
la  Kigongo-Busisi  lenye urefu wa Kilomita 3.2 kwenye sherehe
iliyofanyika eneo la Kigongo jijini Mwanza leo Desemba 7, 2019.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe
Magufuli akiangalia picha kubwa ya mfano wa  Daraja la Busisi-Kigongo
lenye urefu wa Kilomita 3.2 baada ya kuweka jiwe la msingi na kuzindua
rasmi kuanza kwa ujenzi wake kwenye sherehe iliyofanyika Kigongo
jijini Mwanza leo Desemba 7, 2019.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli
akipiga ngoma kwa furaha wakati wa sherehe za uwekaji wa Jiwe la
Msingi la Ujenzi wa Daraja la Busisi-Kigongo lenye urefu wa Kilomita
3.2 kwenye sherehe iliyofanyika Kigongo jijini Mwanza leo Desemba 7,
2019.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimpongeza Waziri wa Ujenzi
Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Isack Kamwelwe mara baada ya
kuweka jiwe la msingi ujenzi wa Daraja hilo la kutoka Kigongo hadi
Busisi mkoani Mwanza.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wanafunzi wa
Shule ya Msingi Inseni B iliyopo Kata ya Butimba mkoani Mwanza.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwapungia mkono wananchi
wa Kigongo na Busisi mara baada ya kuwasili katika eneo la mradi wa
ujenzi wa Daraja hilo refu.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli
akiwa na msichana Salma Yasini, Kiongozi wa wanafunzi wa Shulke ya
msingi ya Iseni B ambaye amemkabidhi shilingi milioni  tano ukiwa ni
mchango wake kusaidia ujenzi wa vyoo na madarasa shuleni hapo
wakitokea kwenye sherehe za uwekaji wa Jiwe la Msingi la Ujenzi wa
Kigongo-Busisi  lenye urefu wa Kilomita 3.2 kwenye sherehe
iliyofanyika Kigongo jijini Mwanza leo Desemba 7, 2019.

Mbunge wa Misungwi Mhe Charles Kitwanga akishiriki kwenye ngoma
ya utamaduni ya kucheza na nyoka mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli wakati wa sherehe ya  uwekaji wa
Jiwe la Msingi la Ujenzi wa Daraja la Kigongo-Busisi  lenye urefu wa
Kilomita 3.2 kwenye sherehe iliyofanyika Kigongo jijini Mwanza leo
Desemba 7, 2019.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli
akipongezwa na Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhandisi Robert Gabriel na Mkuu
wa Mkoa wa Kagera Brigedia Jenerali  Marco. E. Gaguti wakati wa
sherehe za uwekaji wa Jiwe la Msingi la Ujenzi wa Kigongo-Busisi
lenye urefu wa Kilomita 3.2 kwenye sherehe iliyofanyika Kigongo jijini
Mwanza leo Desemba 7, 2019

PICHA NA IKULU
Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com