Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akisisitiza jambo wakati akifunga mradi wa ubia kwa maendeleo ya mifumo ya uzalishaji endelevu wa mpunga Afrika chini ya jangwa la Sahara wilaya ya Mvomero mkoani Morogoro, tarehe 2 Novemba 2019. (Picha Zote Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo)
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akisisitiza jambo wakati akifunga mradi wa ubia kwa maendeleo ya mifumo ya uzalishaji endelevu wa mpunga Afrika chini ya jangwa la Sahara wilaya ya Mvomero mkoani Morogoro, tarehe 2 Novemba 2019.
Sehemu ya washiriki wakifatilia hotuba ya Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) wakati akifunga mradi wa ubia kwa maendeleo ya mifumo ya uzalishaji endelevu wa mpunga Afrika chini ya jangwa la Sahara wilaya ya Mvomero mkoani Morogoro, tarehe 2 Novemba 2019. (Picha Zote Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo)
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akisisitiza jambo wakati akifunga mradi wa ubia kwa maendeleo ya mifumo ya uzalishaji endelevu wa mpunga Afrika chini ya jangwa la Sahara wilaya ya Mvomero mkoani Morogoro, tarehe 2 Novemba 2019.
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akiwa katika picha ya pamoja na sehemu ya wataalamu, washiriki na wanufaika wa mradi wa ubia kwa maendeleo ya mifumo ya uzalishaji endelevu wa mpunga Afrika chini ya jangwa la Sahara wilaya ya Mvomero mkoani Morogoro, tarehe 2 Novemba 2019.
Na Mathias Canal, Wizara ya
Kilimo-Morogoro
Serikali
nimewema kuwa katika msimu wa kilimo wa mwaka 2019/20 kwa kushirikiana na sekta
binafsi, imejipanga kuzalisha jumla ya tani 53,608.2 za mbegu mbalimbali.
Wazalishaji
hao ni pamoja na Wakala wa Taifa wa Mbegu (ASA), Vituo vya Utafiti, Magereza na
Sekta binafsi. Aidha, Wizara kupitia Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula
(NFRA) inaendelea na ujenzi wa Mradi wa Kuongeza Uwezo wa Kuhifadhi
Nafaka.
Waziri wa
Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) ameyasema hayo leo tarehe 2 Novemba 2019 wakati akifunga mradi wa ubia kwa
maendeleo ya mifumo ya uzalishaji endelevu wa mpunga Afrika chini ya jangwa la
Sahara wilaya ya Mvomero mkoani Morogoro.
Amesema
kuwa Sanjali na jitihada hizo, Wizara ya Kilimo imeanzisha kitengo cha masoko
ya mazao ya kilimo ambacho kinahusika na kutafuta masoko ndani na nje ya nchi
kwa mazao mbali mbali yanayozalishwa hapa nchini ili mbegu zitakazozalishwa na
kuwa na mafanikio makubwa katika kilimo uweze kuimarisha kipato cha wananchi.
Takwimu
zinaonesha kwamba wastani wa kitaifa wa matumizi ya zana bora za kilimo
umeongezeka hadi kufikia asilimia 20 kwa matrekta na asilimia 27 kwa wanyama
kazi ikilinganishwa na asilimia 14 ya matrekta na asilimia 24 ya wanyama
kazi mwaka 2013.
Amesema
kuwa Kutokana na ongezeko hilo, matumizi ya jembe la mkono yamepungua na kufikia
asilimia 53 kwa mwaka 2018 ikilinganishwa na asilimia 62 kwa mwaka 2013.
Aidha, kupitia Mfuko wa Taifa wa Pembejeo za Kilimo (AGITF) Wizara imeendelea
kutoa mikopo ya pembejeo na zana za kilimo.
Mhe
Hasunga amesema kuwa pamoja na hayo, Wizara kupitia Tume ya Maendeleo ya
Ushirika imeendelea kuimarisha Sekta ya Ushirika kwa kusimamia na kuhamasisha
maendeleo yake hapa nchini ili wakulima waweze kunufaika na matunda ya serikali
ya awamu ya tano inayoongozwa na Mhe Rais wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli
katika usimamizi madhubuti wa sekta ya ushirika.
Ameongeza
kuwa Wizara ya Kilimo imeendelea kuratibu utekelezaji wa mikakati ya maendeleo
ya kilimo hapa nchini kwa kuimarisha huduma za utafiti, upatikanaji na utumiaji
wa pembejeo na zana za kilimo, udhibiti wa visumbufu vya mazao, huduma za
ugani, uongezaji wa thamani na upatikanaji wa masoko.
Waziri
Hasunga amesema kuwa Serikali imeendelea na jitihada mbalimbali za kuhakikisha
inaongeza tija na uzalishaji wa mazao mbalimbali nchini. Jitihada hizo ni
pamoja na Wizara ya Kilimo kupitia Tume ya Taifa ya Umwagiliaji kukamilisha
mapitio ya Mpango Kabambe wa Taifa wa Umwagiliaji ili kubaini maeneo yanayofaa
kwa kilimo cha umwagiliaji kwa kuzingatia Mipango Shirikishi ya Maendeleo ya
Rasilimali za Maji.
Aidha,
Wizara ya Kilimo imeendelea kuanisha maeneo ya kipaumbele ya kuongeza tija kwa
kuimarisha upatikanaji wa pembejeo za kilimo, udhibiti wa visumbufu, matumizi
ya zana bora za kilimo na huduma za ugani; ujenzi na ukarabati wa miundombinu
ya umwagiliaji; ujenzi wa miundombinu ya kuhifadhi mazao ya kilimo na masoko;
kufanya utafiti wa kilimo na kuzalisha teknolojia kwa mazao mbali mbali ukiwemo
mpunga.
Amesema,
Wizara imeanza na itaendelea kuipitia Sera ya Taifa ya Kilimo ya mwaka 2013 na
sheria mbalimbali kwa lengo la kubaini maeneo ambayo yatapaswa kuhuishwa ili
kwenda na hali halisi ya sasa na mwelekeo wa Serikali wa kubadili kilimo chetu
kuwa kilimo cha kibiashara.
Ameongeza
kuwa Mtazamo wa Wizara ni kuwa na Sheria moja itakayosimamia rasilimaliwatu,
matumizi bora ya pembejeo, ardhi ya kilimo na maeneo mengine muhimu.
Aidha,
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) amesema kuwa serikali inatambua na
kulipongeza Shirika la Kilimo na Chakula la Umoja wa Mataifa-FAO, Serikali ya
Venezuela, Halmashauri za Wilaya za Kilosa, Mvomero na Kilombero kwa
utekelezaji wa mradi wa ubia wa maendeleo ya mifumo ya uzalishaji endelevu
wa mpunga Afrika chini ya jangwa la Sahara.
Kwa
upande wake Muwakilishi wa Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa FAO
nchini Tanzania Ndg Fred Kafeero ameipongeza serikali ya Tanzania kwa
kuimarisha ushirikiano na Taasisi za kimataifa katika kuimarisha sekta ya
kilimo.
Ameongeza
kuwa mradi huo kwa upande wa Tanzania ulilenga kujenga mifumo yenye tija na
endelevu katika Afrika ili kuboresha uhakika wa chakula na kuwezesha maendeleo
endelevu kupitia mnyororo wa tahamani wa zao la mpunga miongoni mwa wakulima
watoto hususani vijana.
Aidha amesema
kuwa mradi huo ulilenga kukabiliana na changamoto zinazosababisha uzalishaji
mdogo wa mpunga hapa nchini kwa kutambulisha na kusambaza teknolojia ya kilimo
shadidi cha mpunga kwa kutumia njia kadhia ambazo FAO imetumia katika nchi
nyingine.
Mkutano
huo umehudhuriwa pia na Balozi wa Venezuela kwa Kenya na Tanzania Mhe Jesus
Manzanilla Puppo, Naibu waziri wa kilimo na Ardhi wa serikali ya Venezuela Mhe
Jose Gregorio Aguilers Contreras, Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe Loata Erasto
Olesanare.
MWISHO
0 comments:
Post a Comment