METDO Tanzania

METDO Tanzania

Monday, August 17, 2015

BASATA YALIFUNGULIA SHINDANO LA MISS TANZANIA


Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) limelifungulia shindano la urembo la Miss Tanzania baada ya  wandaaji wake Kampuni ya LINO International Agency Limited kufuata taratibu, kuomba radhi na kuyafanyia kazi baadhi ya mapungufu yaliyojitokeza na kutekeleza masharti aliyopewa.

Itakumbukwa kuwa mnano tarehe 22/12/2014
 
 BASATA liliwaandikia barua LINO International
Agency Limited ya kulisimamisha shindano la Miss Tanzania kwa miaka miwili
(Mwaka 2015 na 2016) na kuwaagiza kujipanga upya na kurekebisha kasoro ambazo
zimekuwa zikijitokeza mara kwa mara.

Mapungufu yaliyobainishwa ni pamoja na; mosi, kutokufuata Sheria, Kanuni na Taratibu za
uendeshaji matukio ya Sanaa nchini, pili kutokuwasilisha nyaraka mbalimbali za shindano lake hususan mikataba ya washiriki. Tatu kutumia mawakala wasiosajiliwa na kupewa vibali vya BASATA.
Miongoni mjwa mapungufu ambayo Kampuni ya LINO imeyafanyia kazi ni kuanza mchakato wa
usajili wa mawakala – BASATA na kufanyia marekebisho kanuni na taratibu za
uendeshaji wa Mashindano ya Urembo ya Miss Tanzania. Aidha, LINO imewasilisha
muundo wa kamati ya uendeshaji wa shindano yenye muelekeo wa kuzingatia jinsia.
Katika kuboresha na kurudisha hadhi ya shindano la Miss Tanzania, LINO International
Agency Limited imepewa kibali cha muda kisichozidi miezi minne (4) kwa ajili ya
maandalizi ya awali ikiwemo kukamilisha usajili wa mawakala katika ngazi zote
husika.

BASATA linapenda kuwafahamisha wadau wote 
 
wa Sanaa hususan wale wa shindano la urembo
 
la Miss Tanzania kwamba Kampuni ya LINO imetekeleza maagizo ya msingi iliyopewa
kama masharti ya kufunguliwa. Na kwamba baada ya kufanyia kazi changamoto
zilizokuwa zimejitokeza BASATA limeyafungulia mashindano ya Miss Tanzania kwa
masharti ya kukamilisha changamoto zilizobakia.

Ni matarajio ya BASATA kwamba kampuni ya LINO itazingatia taratibu zote za uendeshaji wa
matukio ya Sanaa nchini na kwamba haitarudia tena makosa yatakayopelekea
kuliweka shindano hili katika hali ya kushuka hadhi na kuzua sintofahamu katika
jamii.
Sanaa ni kazi, tuipende na kuithamini
Godfrey
Mngereza
KATIBU MTENDAJI
Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com