Mafundi wakifanya kazi ya kuvuta
nyaya katika Kijiji cha Mnekez wilayani Chato, Mkoa wa Geita ikiwa ni
utekelezaji wa Mradi wa Usambazaji umeme vijijini wa Awamu ya Tatu
Mzunguko wa kwanza (REA III).
Zahanati katika Kijiji cha Mutundu
ambayo imefikiwa na miundombinu ya umeme ikiwa ni utekelezaji wa Mradi
wa Usambazaji umeme vijijini wa Awamu ya Tatu Mzunguko wa kwanza (REA
III).
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakala wa
Nishati Vijijini (REA), Wakili Julius Kalolo (wa Tatu kushoto), Kaimu
Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Mhandisi Amos
Maganga (katikati) na Mjumbe wa Bodi ya REA, Dkt Andrew Komba (wa
kwanza kulia) wakiwa mbele ya zahanati katika Kijiji cha Mutundu
wilayani Chato mara baada ya kukagua kazi ya usambazaji umeme kijijini
hapo.
Kazi ya kuvuta nyaya ikifanyika
katika Kijiji cha Kakindo wilayani Chato, Mkoa wa Geita ikiwa ni
utekelezaji wa Mradi wa Usambazaji umeme vijijini wa Awamu ya Tatu
Mzunguko wa kwanza (REA III).
Kazi ya kuvuta nyaya ikifanyika
katika Kijiji cha Kakindo wilayani Chato, Mkoa wa Geita ikiwa ni
utekelezaji wa Mradi wa Usambazaji umeme vijijini wa Awamu ya Tatu
Mzunguko wa kwanza (REA III).
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakala wa
Nishati Vijijini (REA), Wakili Julius Kalolo (katikati), na Mjumbe wa
Bodi ya REA, Dkt Andrew Komba ( wa pili kulia) wakiwa katika Kijiji cha
Kakeneno wilayani Chato ambapo walifika kukagua kazi ya usambazaji
umeme kijijini hapo. Wengine katika picha ni watendaji kutoka REA,
TANESCO na Kijiji cha Kakeneno.
………………….
Na Teresia Mhagama, Geita
Bodi ya Wakala wa Nishati Vijijini
(REA) imeeleza kuridhishwa kwake na utekelezaji wa maagizo iliyoyatoa
kwa Mkandarasi anayefanya kazi ya kusambaza umeme vijijini wilayani
Chato kampuni ya Whitecity Guangdong JV ambayo yalilenga kuongeza kasi
ya usambazaji umeme vijijini.
Hayo yalielezwa na Mwenyekiti wa
Bodi ya REA, Wakili Julius Kalolo tarehe 17 Novemba, 2019, wilayani
Chato, Mkoa wa Geita mara baada ya kukagua kazi za usambazaji umeme
zinazoendelea wilayani humo akiwa ameambatana na Mjumbe wa Bodi hiyo,
Dkt Andrew Komba na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa REA, Mhandisi Amos Maganga.
Alieleza kuwa, maagizo ya Bodi
hiyo yalitolewa Siku 14 zilizopita ambapo Mkandarasi huyo alielekezwa
kutekeleza kazi ambazo alikuwa hajafanya kwenye baadhi ya maeneo ikiwemo
kuchimba mashimo, kusimika nguzo na kuvuta nyaya ili kuweza kuwasha
umeme katika Vijiji alivyopangiwa kupitia mradi wa usambazaji umeme
vijijini wa Awamu ya Tatu Mzunguko wa kwanza (REA III).
” Tulitoa maagizo haya Wiki mbili
zilizopita baada ya kufanya ziara wilayani hapa na kukuta nguzo zimelala
na Mkandarasi alikuwa haonyeshi kama alikuwa na uwezo wa kufanya kazi
kwa kasi tunayotaka lakini baada ya kukagua leo tumeona nguzo
zimesimikwa na nyaya zimeanza kuwekwa kwenye nguzo, hivyo ameweza
kutekeleza maelekezo.” Alisema
Aliongeza kuwa, Mkandarasi huyo
pia ameanza kazi ya kufunga transfoma kwa ajili ya kusambaza umeme kwa
wananchi hivyo Bodi hiyo ilimtaka kuendelea kuongeza kasi ili maeneo
yote muhimu pamoja na wananchi waunganishiwe umeme.
Aidha, Bodi hiyo ilimwelekeza
Mkandarasi huyo kuwasha umeme katika Kijiji cha Kakeneno na ifikapo
mwishoni wa wiki ijayo wananchi wawe wameunganishwa na umeme kwani
miundombinu imeshafika kijijini hapo na wananchi wameshafanya wiring kwenye nyumba zao.
Vilevile, baada ya kukagua kazi ya
usambazaji umeme katika Kijiji cha Mutundu, Bodi hiyo iliagiza umeme
uwashwe tarehe 18 Novemba, 2019 kwani kuna miundombinu yote ya umeme na
kilichobaki ni kuwasha tu umeme.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa
kampuni Whitecity Guangdong JV, Nuhu Mringo alisema kuwa kampuni hiyo
imejitahidi kutekeleza maagizo ya Bodi yaliyotolewa Wiki mbili
zilizopita na kuahidi kuendelea kutekeleza kazi hiyo kwa kasi na kwa
viwango.
Ikiwa wilyani Chato, Bodi hiyo
ilikagua kazi ya usambazaji umeme katika Kijiji cha Mutundu, Kakindo,
Kamanga, Mnekez, Kakeneno na Matofali.
0 comments:
Post a Comment