Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akiwa na mfanyabiashara wa pembejeo Ndg Lukas Simkonda wakati akiwa katika ziara ya kikazi ya ukaguzi wa upatikanaji wa mbolea katika kijiji cha Ipunda mkoani Songwe, leo tarehe 21 Novemba 2019. (Picha Zote Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo)
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akikagua kiwanda kidogo cha ubanguaji karanga wakati akiwa katika ziara ya kikazi ya ukaguzi wa upatikanaji wa mbolea katika kijiji cha Ipunda mkoani Songwe, leo tarehe 21 Novemba 2019.
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akizungumza na wananchi waliofika kutibiwa katika zahanati ya Ipunda wakati akiwa katika ziara ya kikazi ya ukaguzi wa upatikanaji wa mbolea katika kijiji cha Ipunda mkoani Songwe, leo tarehe 21 Novemba 2019.
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akikagua karanga zilizobanguliwa katika kiwanda kidogo cha ubanguaji karanga wakati akiwa katika ziara ya kikazi ya ukaguzi wa upatikanaji wa mbolea katika kijiji cha Ipunda mkoani Songwe, leo tarehe 21 Novemba 2019.
Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Songwe
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) leo
tarehe 21 Novemba 2019 amefanya ziara ya kushitukiza ili kujionea hali ya
upatikanaji wa mbolea katika baadhi ya vijiji mkoani Songwe.
Katika ziara hiyo Mhe Hasunga kadhalika
amekagua na kujionea kama wafanyabiashara wanauza mbolea kutokana na maelekezo
ya serikali iliyopanga bei elekezi na kuitangaza hivi karibuni.
Akiwa katika ziara hiyo ya kikazi katika
kijiji na Kata ya Ipunda katika Halmashauri ya Wilaya ya Mbozi Mhe Hasunga
amempongeza mfanyabiashara wa pembejeo kijijini hapo Ndg Lukas Simkonda kwa
kuuza mbolea kwa gharama ya chini kuliko bei elekezi.
“Wewe ni miongoni mwa wafanyabiashara
tunaowataka, serikali imepanga bei elekezi lakini wewe umeamua kuuza chini ya
bei elekezi ili kuwanufaisha zaidi wakulima, jambo hili sisi kama serikali
tunaliunga mkono na kukupongeza kwa dhati kwa kazi ya kizalendo unayoifanya”
Alisisitiza Mhe Hasunga
Katika hatua nyingine Wafanyabiashara wa mbolea
nchini wametakiwa kuuza bidhaa hiyo kwa kufuata bei elekezi zilizotangazwa na
Waziri wa Kilimo hivi karibuni kwani lengo la serikali ni kuhakikisha wakulima
wanapata mbolea ya uhakika na kwa bei nafuu.
Aliitaja sababu ya
kuwa na bei elekezi ya mbolea kuwa ni kukuza kilimo na kuongeza mavuno ya mazao
ambayo ndio malighafi kuu inayohitajika wakati huu ambapo serikali inatekeleza
mipango ya ukuaji wa viwanda, kama msingi mkuu wa uchumi.
Katika ziara hiyo Mhe Hasunga akiwa katika
zahanati ya Ipunda katika Jimbo lake la uchaguzi la Vwawa amewapongeza wakazi
wa kijiji hicho kwa kujitokeza kwa wingi kupima Virusi vya UKIMWI na UKIMWI kwani
amesema kupima afya ni msingi wa uimarishaji wa afya zao.
Vilevile Mhe Hasunga amewataka wakulima kula
chakula kizuri chenye mchanganyiko wa mbogamboga na matunda. “Wakulima wangu
mnaniangusha maana ninyi mnalima na kuzalisha chakula cha kutosha lakini ajabu
ninyi ndio mnaongoza kutokula vizuri jambo hili sio sahihi kabisa, mnapaswa
kuimarisha afya zenu kwa kula vizuri” Alisema Mhe Hasunga
Katika hatua nyingine Waziri Hasunga
amewapongeza wajasiriamali Wilayani Mbozi kwa kuanzisha viwanda vidogo vya
ubanguaji wa karanga kwani vitaongeza uwezekano wa wakulima kuongeza uzalishaji
wa karanga kwakuwai nyenzo za kubangua zitakuwepo kutokana na teknolojia hiyo
ya kisasa.
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga ambaye ni
Mbunge wa Jimbo la Vwawa Mkoani Songwe ameanza ziara ya kikazi ya siku 6 mkoani
humo ambapo pamoja na mambo mengine anakagua hali ya upatikanaji wa mbolea
pamoja na kukagua kama wafanyabiashara wanauza mbolea kutokana na bei elekezi
iliyowekwa na serikali.
MWISHO
0 comments:
Post a Comment