METDO Tanzania

METDO Tanzania

Wednesday, November 20, 2019

MAADHIMISHO YA SIKU YA HAKI ZA WATOTO DUNIANI


Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili, Mhe. Ally Hassan Mwinyi (katikati),
akifurahia jambo na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na
Watoto, Dkt. Faustine Ndungulile (kushoto) na Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya
Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Ally Possi, mara baada ya kuwasili
katika Maadhimisho ya Siku ya Haki ya Mtoto Duniani iliyofanyika katika Kituo cha
Mikutano cha Kimataifa Julius Nyerere.
Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili, Mhe. Ally Hassan Mwinyi, baada ya kuwasili
katika Sherehe za Kuadhimisha ya Siku ya Haki ya Mtoto Duniani iliyofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Julius Nyerere, leo Novemba 20, 2019, ambako
alialikwa kuwa mgeni Rasmi.
Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili, Mhe. Ally Hassan Mwinyi, akipata maelezo
kutoka kwa mtalaam kutoka Shirika la Watoto Duniani (UNICEF), katika moja ya
banda lililokuwepo kwenye Maadhimisho ya Siku ya Haki ya Mtoto Duniani
iliyofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Julius Nyerere.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na
Watoto, Dkt. Faustine Ndungulile, akizungumza na Washiriki wa Sherehe za
Maadhimisho ya Siku ya Haki ya Mtoto Duniani iliyofanyika katika Kituo cha
Mikutano cha Kimataifa Julius Nyerere.
Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt.
Ally Possi, akizungumza na Washiriki wa Sherehe za Maadhimisho ya Siku ya Haki ya
Mtoto Duniani iliyofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Julius Nyerere.
Mwanafunzi kutoka Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Kampala mwaka wa
Tatu, Rose Mweleka, akiwasilisha mada kuhusu jinsi ya kutekeleza haki za watoto wa kike ikiwemo kuwafundisha hatua za makuzi ili kuwawezesha kukabiliana na hali wakifikia umri husika, Mada hiyo iliwasilishwa kwenye Maadhimisho ya Siku ya Haki ya Mtoto Duniani iliyofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Julius
Nyerere.
Wanafunzi wakionyesha bango lenye ujumbe wa haki za watoto mara baada ya kuzindua ajenda kuhusu haki za watoto uliofanyika kwenye Maadhimisho ya Siku ya Haki ya Mtoto Duniani iliyofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Julius Nyerere.
Watoto kutoka Shule mbalimbali za Jijini Dar es Salaam, wakiwa katika
picha ya pamoja na Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili, Mhe. Ally Hassan Mwinyi, na
viongozi wengine wa Serikali katika Maadhimisho ya Siku ya Haki ya Mtoto Duniani
iliyofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Julius Nyerere.
Watoto kutoka Kikundi cha Safi Theater cha Jijini Dar es Salaam, wakionesha jinsi watoto wa shule wanavyofanyiwa ukatili wa kijinsia na waendesha Bodaboda na Daladala na kukatishwa masomo, igizo lilitolewa katika Maadhimisho ya Siku ya Haki ya Mtoto Duniani iliyofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Julius Nyerere.

Picha na Idara ya Habari-MAELEZO
Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com