Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu,
Bw. Jumanne Sagini akifungua mafunzo kwa viongozi, wataalam wa Kilimo
na ushirika mkoa wa Simiyu yaliyoandaliwa na Shirika la Bima la
Taifa(NIC), yaliyofanyika Novemba 07, 2019 Mjini Bariadi kwa lengo la
kujenga uelewa wa pamoja juu ya Bima ya Mazao inayotarajiwa kutolewa kwa
wakulima wa pamba mkoani Simiyu.
Mratibu wa Bima ya mazao kutoka
Shirika la Bima la Taifa (NIC), Bw. Prosper Peter akitoa mada kwenye
mafunzo kwa viongozi, wataalam wa Kilimo na ushirika mkoa wa Simiyu
yaliyoandaliwa na Shirika la Bima la Taifa(NIC), yaliyofanyika Novemba
07, 2019 Mjini Bariadi kwa lengo la kujenga uelewa wa pamoja juu ya Bima
ya Mazao inayotarajiwa kutolewa kwa wakulima wa pamba mkoani Simiyu.
Baadhi ya viongozi wa Serikali na
wataalam wa kilimo na ushirika wakimsikiliza Mratibu wa Bima ya mazao
kutoka Shirika la Bima la Taifa (NIC), Bw. Prosper Peter(hayupo
pichani) kwenye mafunzo kwa viongozi, wataalam wa Kilimo na ushirika
mkoa wa Simiyu yaliyoandaliwa na Shirika la Bima la Taifa(NIC),
yaliyofanyika Novemba 07, 2019 Mjini Bariadi kwa lengo la kujenga uelewa
wa pamoja juu ya Bima ya Mazao inayotarajiwa kutolewa kwa wakulima wa
pamba mkoani Simiyu.
Mkuu wa Wilaya ya Itilima, Mhe.
Benson Kilangi akichangia hoja katika mafunzo kwa viongozi, wataalam wa
Kilimo na ushirika mkoa wa Simiyu iliyoandaliwa na Shirika la Bima la
Taifa(NIC), yaliyofanyika Novemba 07, 2019 Mjini Bariadi kwa lengo la
kujenga uelewa wa pamoja juu ya Bima ya Mazao inayotarajiwa kutolewa kwa
wakulima wa pamba mkoani Simiyu.
Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe.
Festo Kiswaga akichangia hoja katika mafunzo kwa viongozi, wataalam wa
Kilimo na ushirika mkoa wa Simiyu iliyoandaliwa na Shirika la Bima la
Taifa(NIC), yaliyofanyika Novemba 07, 2019 Mjini Bariadi kwa lengo la
kujenga uelewa wa pamoja juu ya Bima ya Mazao inayotarajiwa kutolewa kwa
wakulima wa pamba mkoani Simiyu
……………………
Na Stella Kalinga, Simiyu
Shirika la Bima la Taifa
(NIC)linatarajia kuanza kutoa huduma za bima ya mazao kwa wakulima wa
pamba katika Wilaya ya Meatu na Maswa Mkoani Simiyu, ambapo wakulima
watakuwa na uwezo wa kukata bima katika zao la pamba itakayomkinga dhidi
ya majanga ukame,mvua zilizozidi kiasi , mafuriko, moto pori ,magonjwa
na wadudu wasiothibitika.
Hayo yamebainishwa na Mratibu
wa Bima ya mazao kutoka Shirika la Bima la Taifa (NIC), Bw. Prosper
Peter wakati akitoa mafunzo kwa viongozi, wataalam wa Kilimo na
ushirika mkoa wa Simiyu yaliyoandaliwa na NIC yaliyofanyika Novemba 07,
2019 Mjini Bariadi kwa lengo la kujenga uelewa wa pamoja juu ya Bima ya
Mazao inayotarajiwa kutolewa kwa wakulima wa pamba mkoani Simiyu.
“Huduma ya bima ya mazao itaanza
kwanza na kumkinga mkulima dhidi ya majanga kama vile ukame , mvua
zilizozidi kiasi , mafuriko, moto pori,magonjwa na wadudu wasiothibitika
na itakatwa kwa pamoja kwa hiyo tutakuwa tunakinga mtaji wa mkulima
aliouwekeza katika kilimo,” alisema Peter.
Aidha, Peter amesema pamoja na
bima kukinga mtaji wa mkulima katika uzalishaji, NIC kwa kushirikiana
na Wizara ya Kilimo itaendelea kuboresha na kuongeza wigo wa huduma za
bima ya mazao kwa kuangalia mahitaji ya wakulima wa pamba kwa wakati
husika ikiwemo suala la bei.
Awali akifungua mafunzo Katibu
Tawala mkoa wa Simiyu,Bw, Jumanne Sagini amesema wakulima wanakabiliwa
na changamoto mbalimbali ikiwemo upatikanaji wa pembejeo, mvua iliyozidi
hivyo Bima itawahakikishia kupata fidia pale wanapopata hasara
inayosababishwa na changamoto hizo na kusisitiza viongozi na wataalam
kutoa ushirikiano kwa NIC wanapotekeleza
Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya
Itilima, Mhe. Benson Kilangi amesema kuwa ujio wa bima ya mazao ni wa
msingi hivyo ni vema NIC ikatoa bima kwa mahitaji/changamoto ambayo ni
ya kipaumbele katika eneo fulani kwa kuwa changamoto za wakulima
zinatofautiana, huku akitolea mfano kwa mkoa wa Simiyu kuwa ukame hauna
athari sana kwenye zao la pamba.
Afisa kilimo wa Halmashauri ya
Mji wa Bariadi, Bibi. Suzana Sabuni amesema kuwa ni vyema bima hiyo
ijikite kwenye vipaumbele vya wakulima kutokana na mazao wanayolima
ikiwa ni sambamba na kuwapata uhuru wakulima kuchagua bima wanayoitaka.
Naye afisa ushirika kutoka
wilaya ya Itilima Heri Muhina ameshauri kuwa katika upande wa majanga ni
vyema bima ilenge kuwasaidia katika majanga ya moto ambayo yamekuwa
yakitokea kwenye baadhi ya maghala ya vyama vya ushirika (AMCOS) pindi
wakulima wanapokuwa wamehifadhi pamba yao.
Akifunga kikao hicho mkuu wa
wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga amesema kuwa ni vyema utekelezaji
huo uanze mapema kuelekea msimu mpya wa kilimo wa mwakani 2019/ 2020 na
kusisitiza wakulima wapate taarifa sahihi kwa wakati ili waweze
kuifahamu vizuri kabla ya utekelezaji.
0 comments:
Post a Comment