Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni,
Sanaa na Michezo Juliana Shonza akifungua tamasha la michezo la wiki ya
kuzuia na kudhibiti magonjwa yasiyo ambukiza leo jijini Dodoma ambapo
kilele chake ni Novemba 14, 2019 ambapo Mgeni Rasmi anatarajiwa kuwa
Waziri Mkuu wa Jahuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Mjaliwa.
Naibu Waziri wa Habari,
Utamaduni, Sanaa na Michezo Juliana Shonza akito vifaa vya michezo
mbalimbali wakatimwa ufunguzi wa tamasha la michezo la wiki ya kuzuia na
kudhibiti magonjwa yasiyo ambukiza leo jijini Dodoma.
Venance Mwamoto Mbunge wa Kilolo
ni akiendelea na mazoezi kabla ya ufunguzi wa tamasha la michezo la wiki
ya kuzuia na kudhibiti magonjwa yasiyo ambukiza leo jijini Dodoma
wakati timu ya Bunge akijiandaa na mchezo dhidi ya watumishi wa umma leo
katika uwanja wa Jamhuri Dodoma.
Katibu Mkuu Wazara ya Habari,
Utamaduni, Sanaa na Michezo Bi. Suzan Mlawi (wa pili kushoto) akishiriki
mazoezi wakati wa ufunguzi wa tamasha la michezo la wiki ya kuzuia na
kudhibiti magonjwa yasiyo ambukiza leo jijini Dodoma. Wa pili kulia ni
Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto
Naibu Katibu Mkuu (Afya) Dkt. Zainabu Chaula.
Watumishi wa Umma waliendelea na
mazoezi mbalimbali leo uwanja wa Jamhuri Dodoma wakati wa ufunguzi wa
tamasha la michezo la wiki ya kuzuia na kudhibiti magonjwa yasiyo
ambukiza.
(Picha na Eleuteri Mangi, WHUSM, Dodoma)
……………..
Na Eleuteri Mangi, WHUSM, Dodoma
Waajiri wametakiwa kuboresha
mazingira ya kazi kwa kuhakikisha watumishi wanashiriki katika michezo
na kufanya mazoezi maeneo yao ya kazi.
Rai hiyo imetolewa na Naibu Waziri
wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Juliana Shonza leo wakati wa
ufunguzi wa tamasha la michezo la wiki ya kuzuia na kudhibiti magonjwa
yasiyo ambukiza linalofanyika katika uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma
ambapo kilele chake ni Novemba 14, 2019 ambapo Mgeni Rasmi anatarajiwa
kuwa Waziri Mkuu wa Jahuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Mjaliwa.
“Mnaweza kuanzisha timu
mbalimbali za michezo na kutenga siku maalum katika mwezi kwa ajili ya
mabonanza ya michezo kwa kuweka mazingira rafiki ya kufanyia mazoezi
kazini kwa kununua vifaa na kutenga vyumba vya mazoezi. Hii itaimarisha
afya za watumishi na kupunguza gharama za matibabu katika taasisi
husika.” Naibu Waziri Juliana Shonza.
Naibu Waziri Shonza amesema kuwa
tamasha hilo linalenga kuhamasisha wananchi kushiriki katika michezo
mbalimbali na mazoezi ya viungo ili kukabiliana na magonjwa
yasiyoambukiza ambayo yamekuwa yakiongezeka hapa nchini.
Magonjwa yasioyoambukiza hutokana
na mitindo isiyofaa ya maisha kama matumizi ya tumbaku, lishe duni,
matumizi ya pombe kupita kiasi, pamoja na kutoshughulisha mwili au
kutofanya mazoezi ya viungo mara kwa mara.
Magonjwa hayo ni kisukari,
shinikizo la juu la damu, magonjwa ya moyo na mishipa, saratani, pumu
na magonjwa ya akili ambayo yamekuwa sugu na yana gharama kubwa za
matibabu ambapo amesema kuwa watu wengi hufikiria mazoezi ni lazima
ukimbie au ucheze mpira, la hasha. Mazoezi ni jambo lolote linalohusisha
misuli na kusababisha kuongezeka kwa mapigo ya moyo na kasi ya
kupumua.
Wataalam wa afya wanasema kuwa
kiwango cha mazoezi kinacholeta faida ni mazoezi yasiyopungua dakika 30
kwa siku angalau siku tatu kwa wiki na yanayomfanya mtu kutokwa na
jasho.
Aidha, Naibu Waziri amesisitiza
kuwa kupitia tamasha hilo, ufanyike uhamasishaji wa watu kupima afya
hususani wa magonjwa yasiyoambukiza. Tiba ya mapema inapunguza uwezekano
wa kupatwa na madhara zaidi.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya
Chemba Saimon Odunga ambaye alimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt.
Binilith Mahenge amewakaribisha washiriki wa tamasha hilo mkoani Dodoma
ambalo limeshirikisha washiriki kutoka ndani na nje ya mkoa huo na hata
nje ya nchi.
Odunga amewataka wakazi na
wananchi wa mkoa wa Dodoma kutumia fursa ya tamasha hilo kwa kushiriki
michezo mbalimbali hatua ambayo itwasaidia watu na jamii nzima kuweka
afya zao katika hali bora ambayo inawatenga na magonjwa yasiyoambukiza.
Tamasha hilo ni la wiki moja
ambalo limeandaliwa na kuratibiwa na Wizara ya Afya, Maendeleo ya
Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwa kushirikiana na Wizara ya Habari,
Utamaduni, Sanaa na Michezo Sekretarieti ya Mkoa wa Dodoma, pamoja na
Wizara ya Ofisi ya Rais TAMISEMI ambapo limeshirikisha michezo
mbalimbali ikiwemo mpira wa miguu, pete, kikapu pamoja mchezo wa kuvuta
kamba. Tamasha hilo linaongozwa na kauli mbiu yetu ya mwaka huu;
“Tutembee Pamoja Katika Kuzuia na Kudhibiti Magonjwa Yasiyoambukiza”
0 comments:
Post a Comment