Mkuu wa Mkoa wa Songwe Brig. Jen.
Nicodemus Mwangela akionyesha Kitabu cha Mpango wa Miaka mitano wa
maendeleo ya Miundombinu ya Mahakama ya Tanzania ambacho amekabidhiwa
mapema leo na Jaji Mkuu wa Tanzania Profesa Ibrahim Juma.
Jaji Mkuu wa Tanzania Profesa
Ibrahim Juma (mwenye tai nyekundu) akikagua ramani ya eneo ambapo
itajengwa Mahakama ya Mkoa katika kijiji cha Selewa Wilaya ya Mbozi
mapema leo alipotembelea Mkoa wa Songwe.
Mkuu wa Mkoa wa Songwe Brig. Jen. Nicodemus Mwangela akisalimiana na Jaji Mkuu wa Tanzania Profesa Ibrahim Juma (mwenye tai nyekundu) mapema leo katika eneo la Mahakama ya Mwanzo Mlowo.
************************************
Jaji Mkuu wa Tanzania Profesa
Ibrahim Juma amefanya ziara ya siku Moja Mkoani Songwe na kumkabidhi
Mkuu wa Mkoa wa Songwe Brig. Jen. Nicodemus Mwangela Mpango wa Miaka
mitano wa maendeleo ya Miundombinu ya Mahakama ya Tanzania.
Makabidhiano hayo
yamefanyika mepama leo katika Ofisi ya Hakimu wa Mkoa wa Songwe iliyopo
Vwawa ambapo Profesa Juma amesema Mpango huo utamwezesha Brig. Jen.
Mwangela kusaidia kusukuma na kufuatilia utekelezaji wake.
Profesa Juma
amesema ziara yake imelenga kuona Changamoto ambazo Mahakama inazo kwa
Mkoa wa Songwe na kwakuwa Mkoa huu ni Mpya, wameuweka katika mipango yao
kwakuwa kila sehemu yenye changamoto imewekewa ratiba ya utekelezaji.
“Bila kuweka
Mpango Mkakati na kupanga lini unafanya nini, utajikuta hakuna chochote
kitakacho onekana kinafanyika, kwahiyo ninakukabidhi Mpango wa Miaka
Mitano wa Maendeleo ya miundombinu ya Mahakama ya Tanzania, si kwa hapa
Mkoani tu hadi katika Wilaya za Mkoa wa Songwe.”, amesema Profesa Juma.
Katika ziara yake
Profesa Juma ametembelea Mahakama ya Mwanzo ya Mlowo, amekagua eneo
itakapojengwa mahakama ya Mkoa katika kijiji cha Selewa Wilayani Mbozi
na kutembelea Mahakama ya Mkoa iliyopo Vwawa.
Mkuu wa Mkoa wa
Songwe Brig. Jen. Nicodemus Mwangela amemshukuru Profesa Juma kwa
kutembelea Mkoa wa Songwe na ana matuamini kuwa Miundo mbinu ya Mhakama
Mkoani hapa itaboreshwa.
0 comments:
Post a Comment