Joyce Mujuru
Aliyekuwa
makamu wa rais wa Zimbabwe Joyce Mujuru anasema kuwa atafurahia kubuni
muungano na chama cha upinzani cha MDC ili kumuondoa madarakani rais
Robert Mugabe.
Bi Mujuru
ameiambia BBC kwamba yuko tayari kufanya kazi na chama cha Movemnet for
Democratic Change kinachoongozwa na Morgan Tsvangira na wengine kwa
niaba ya raia wa taifa hilo.
Alizndua
rasmi chama chake mapema mwaka huu baada ya kufutwa kazi kama makamu wa
rais kabla ya kufukuzwa katika chama tawala cha ZANU PF .
Rais Mugabe mwenye umri wa miaka 92 amesema kuwa atawania muhula mwengine katika uchaguzi ujao.
Kumekuwa na maandamano katika wiki za hivi karibuni kuhusu hali mbaya ya kiuchumi nchini Zimbabwe.
BBC
0 comments:
Post a Comment